Loading...
 

Klabu za Manufaa ya Umma

 

Klabu za Manufaa ya Umma 

Kwa masuala ya kesi kwa kesi, Agora Speakers International inaweza ikaipa klabu vizuizi vya uanachama, lakini ambavyo ni kwa ajili ya manufaa kwa ujumla kama Klabu ya Manufaa ya Umma (PIC). Hii inaweza kutokea kama vizuizi hivi vinginevyo visingekubaliwa. 

Klabu za Manufaa ya Umma hailipi ada yoyote kwa Agora Speakers International lakini inaweza ikazuia uanachama na mahudhurio kutokana na asili yake maalum.  

Baadhi ya mifano ya Klabu za manufaa ya Umma ni:

  • Klabu ndani ya asasi za kiserikali ambazo zinahudhuriwa na wafanyakazi wa serikali.
  • Klabu ndani ya shule na vyuo vikuu ambazo zinahudhuriwa na wanafunzi, walimmu, na/au wazazi. 
  • Klabu ndani ya hospitali, vituo vya kulelea watoto, hospitali za wagonjwa mahututi, vituo vya watoto yatima, nyumba za wazee, nk. 
  • Klabu ndani ya magereza/jela. 

Kwa ujumla, PIC lazima wakutane kwenye eneo la taasisi iliyo mwenyeji wao, kwasababu inadhaniwa ni kwa manufaa ya taasisi kuwa na aina hiyo ya klabu. Kwahiyo taasisi inania ya kutoa msaada wa miundombinu. Kwa mfano, klabu kwa ajili ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Columbia ambao wanakutana katika bar mjini New York haiwezi kuwa na hadhi ya PIC. 

Isipokuwa kwenye kesi ambazo wanachama wa klabu wanahitaji kulindwa au wanazuiliwa kuwasiliana na dunia ya nje (kwa mfano, kwa sababu za kiafya au usalama), PIC zote lazima zikutane uso kwa uso mara kwa mara (lakini, mara chache kwenye mikutano ya mitandaoni inakubaliwa). Tukiendelea na mfano wa hapo juu, klabu ya mtandaoni ya Chuo Kikuu cha Columbia haiwezi kuwa na hadhi ya PIC.

Tafadhali kumbuka, kwa ujumla, tunahitaji mashirika ambayo yatakuwa waenyeji wa klabu kutokuwa na ubaguzi na wanaendana na sheria ndogo za Agora (japokuwa kunaweza kuwa na vigezo vya utofauti kwenye masuala maalum, kama klabu ndani ya gereza la jinsia moja au kundi la walionusurika unyanyasaji wa nyumbani). 

Utaratibu wa Kujiandikisha 

Kuomba hadhi ya PIC, tafadhali jiandikishe kama klabu yenye Vizuizi kwanza, ukieleza unataka kuomba hadhi ya PIC. 

Kutegemea na aina ya shirika ambayo litakuwa ni mwenyeji wa klabu, utahitaji pia kututumia kielektroniki nyaraka zifuatazo: 

  • Kwa PIC ambazo zipo ndani ya mashirika ya kielimu ambayo yanatambulika rasmi: 
    • Jina kamili, anuani kamili ya mahali ilipo, na ya taasisi ambayo itakuwa mwenyeji wa klabu. 
    • Klabu itakutana mahali gani (ikiwemo jengo na chumba maalum) lazima iwepo kwenye eneo la taasisi. 
       
  • Kwa PIC ambazo zipo ndani ya asasi za kiserikali, mashirika ya kiafya, vituo vya kulea watoto, hospitali za wagonjwa mahututi, vituo vya watoto yatima, nyumba za wazee, na magereza:
    • Jina kamili, anuani kamili ya mahali ilipo, na ya taasisi ambayo itakuwa mwenyeji wa klabu. 
    • Tovuti ya shirika. 
    • Barua ya kuidhinisha ambayo imesahihiwa na mtu anayehusika ndani ya taasisi inayoruhusu uundwaji wa klabu. Barua lazima iwe na jina kamili na taarifa za mawasiliano za moja kwa moja (zote za barua pepe ya taasisi na namba ya simu) ya mtu anayehusika. Tafadhali kumbuka kuwa tunahitaji barua pepe na namba ya simu ya moja kwa moja, na sio barua pepe ya kawaida ya taasisi. Barua pepe lazima iwe na miliki "domain" ya taasisi. Kama lugha ya barua ya kuidhinisha sio Kiingereza au Kihispania, tutahitaji itafsiriwe kwenda moja ya lugha hizo na iwe na muhuri wa wakili. 
       
  • Kwa PIC ambazo zipo ndani ya mashirika mengine:
    • Nyaraka zote ambazo zimetajwa juu, jumlisha:
    • Barua kutoka mwanzilishi wa klabu akielezea kwanin wanaamini kuwa klabu inafanya huduma ya kijamii.
    • Sheria ndogo zilizopo au hati ya taasisi ambayo klabu inakutana, kwenye lugha yake halisi na iliyotafsiriwa kwenda Kiingereza.

 

Kama hadhi ya PIC haitotolewa...

Kama uliomba hadhi ya PIC na haikutolewa, una chaguo zifuatazo:

  • Fanyia kazi masuala yaliyotajwa kwenye barua ya maamuzi na uombe tena. 
  • Iache klabu kuwa ya Vizuizi, ukilipa ada inayohusika. 
  • Badilisha klabu kuwa klabu ya Umma, ukiondoa vizuizi vya uanachama. 

Kama hadhi ya PIC itatolewa...

Hongera! Klabu sasa inaweza kufurahia bila gharama zozote faida zote ambazo Agora inatoa. 

Adiha "PIC" au "Klabu za Manufaa ya Umma" kiambishi-tamati kitaongezewa kwenye jina la klabu kwenye nyaraka zote rasmi za Agora. (Kwa mfano, "Wazungumzaji wa PapoHapo PIC" au "Wazungumzaji wa Agora PIC"). Kwasababu C kwenye PIC tayari inaamisha "Klabu", kama jina la mwanzo tayari lilijumuisha neno "Klabu", jina litabadilika ipasavyo ("Klabu ya Wazungumzaji Bora" itabadilika kuwa aidha "Wazungumzaji Bora PIC" au "Wazungumzaji  Bora Klabu ya Manufaa ya Umma",  kwa chaguo lako).

Kwa ujumla, hadhi ya PIC haina kikomo cha muda, kwahiyo hamna haja ya kufanya utaratibu wowote ili kuipata upya tena. Lakini, kama taarifa zozote ambazo zimetumiwa wakati wa kuomba hadhi ya klabu ya manufaa ya umma zikiacha kuwa halali (zikiwa batili), unahitaji kuwasilisha toleo mpya. Kwa mfano, kama mtu ambaye aliidhinisha kuunda kwa klabu hafanyi kazi tena kwenye shirika mwenyeji, barua mpya ya kuidhinisha inatakiwa itiwe sahihi na mfanyakazi/ofisa mpya. 

Kuhakikisha kuwa mfumo wa PIC hautumiwi vibaya, Agora Speakers International inaweza mara chache kufanya uhakiki au ukaguzi wa hadhi ya klabu za manufaa ya umma na wanaweza wakaulizia nyaraka za ziada. Kama kuna vitu ambavyo havipo sawa vitapatikana, klabu itapewa muda maalum wa kuvieleza. Kama havitoelezea, hadhi ya klabu ya manufaa ya umma itaondolewa. 

Mahali pa Mkutano

Klabu za Manufaa ya Umma zina uhuru wa kuchagua mahali popote wanapotaka kwa ajili ya mikutano, maadam haziongezi safu nyingine ya ubaguzi kwa wanachama. 

 

Wageni na Wanaozuru

Klabu za manufaa ya umma zinatakiwa kukubali kutembelewa na maofisa wa Shirika la Agora Speakers International na wanachama wa Bodi ya Wakurugenzi wa Agora Speakers International kwa ajili ya ukaguzi, uadilifu, na ukurufunzi/ushauri, wakipita hatua zote za lazima za ulinzi kwenye mahali pa mkutano/ukumbi. 

Kama wakitaka, klabu za PIC wanaweza wakakubali wageni kutoka makundi mengine, kama vile mabalozi wa Agora, wanachama wengine wa klabu za Agora, nk.

 

Vigezo vya Kifedha

Klabu za Manufaa ya Umma haziruhusiwi kutoza ada kwa wanachama wake, kwasababu inadhaniwa kuwa shirika linalowalea linalipa gharama zao zote. 

Kwasababu hamna ada zozote, hamna haja ya vigezo vya kurepoti, aidha.

 

Taarifa za Kuorodhesha

Taarifa zifuatazo za Klabu za Manufaa ya Umma zinasambazwa, na lazima maofisa wa klabu wahakikishe ni za hivi karibuni. 

 

taarifa za klabu za kusambazwa 
Aina ya Taarifa Zinasambazwa kwa 
Jina la klabu, namba na siku ya kuanzishwa Hadhira
Ratiba ya mkutano Mabalozi wa Agora na maofisa wa shirika la Agora
Mahali pa Mkutano Hadhira
Maofisa wa klabu na taarifa zao za mawasiliano Mabalozi wa Agora na maofisa wa shirika la Agora 
Muundo wa ada Haihusiani 
Fedha za klabu Faragha  (haina haja ya usimamizi wa Agora)
Vizuizi vya Kuzuru Hadhira
Vizuizi vya Maudhui ya Hotuba Hadhira
Taarifa za mawasiliano za klabu Hadhira
Tuzo na Medali Hadhira
Lugha za Klabu Hadhira
   

 

Uangalizi wa Muundo wa Kielimu wa Agora 

Kuhusu uangalizi wa Muundo wa Kielimu wa Agora, Klabu za Manufaa ya Umma zinafuata masharti sawa na Klabu za Umma, isipokuwa ya haya yafuatayo: 

  • Ukiachana na maudhui ya hotuba kwa ujumla ambayo Klabu za Umma imeanzisha, klabu za manufaa ya umma wanaweza wakaongeza kizuizi kwenye maudhui ya hotuba ya mada kwa uanachama ilimradi vizuizi hivi vinahusiana kwa uwazi na vizuizi vya uanachama. 
  • Inaruhusiwa kutangaza asasi au shirika ya kitaaluma ambayo yanakuwa kama kigezo cha uanachama. Kwa mfano, kama klabu ni ya wataalam wa IT (teknolojia ya habari na mawasiliano) tu ambao ni wa ACM, ni sawa kutangaza ACM ndani ya klabu. 

Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:44 CEST by agora.