Loading...
 

Klabu za Shirika

 

José Manuel Ropero Tagua, mwanzilishi wa klabu ya kwanza ya shirika ya Agora akiwa RSI, akizungumza kuhusu safari aliyopitia katika Kongamano la Kimataifa la 2019.
José Manuel Ropero Tagua, mwanzilishi wa klabu ya kwanza ya shirika ya Agora akiwa RSI, akizungumza kuhusu safari aliyopitia katika Kongamano la Kimataifa la 2019.

 

Uanachama

Klabu ambazo zipo ndani ya shirika jingine (la biashara au sio la kibiashara) ni kwa ajili ya wafanya kazi au wanachama wa shirika tu.

Shirika hilo halitakiwi kujishughulisha na vitendo ambavyo vipo dhidi ya kanuni za msingi au sheria za shirika.

Klabu za shirika sio lazima ziwe na kizuizi cha umri. Kwa maneno mengine, kuwa na "klabu ya vijana ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni X" sio aina ya klabu ambayo inaruhusiwa. Badala yake, klabu inatakiwa ipewe jina la klabu ya umma ya vijana.

Mahali pa mkutano

Klabu za shirika lazima zikutane kwenye eneo la shirika au kwenye ukumbi ambao limetolewa na shirika.

Wageni na Wanaozuru   

Klabu za shirika zinatakiwa kukubali kutembelewa na maofisa wa Shirika la Agora Speakers International na wanachama wa Bodi ya Wakurugenzi wa Agora Speakers International kwa ajili ya ukaguzi, uadilifu, ukurufunzi/ushauri, wakipita hatua za lazima za usalama ndani ya ukumbi.

Vigezo vya Kifedha     

Klabu za shirika haziripoti fedha zake kwa Agora Speakers International na wanashughulikia masuala yao ya ndani jinsi wanavyoona inayofaa.

Tofauti na Klabu za Umma, klabu za shirika zinalipa ada kwa Agora Speakers International, kama ifuatavyo:

  • Ada ya $100 ya kuanzisha.
  • Ada ya $50 kila mwaka kwa kila mwanachama, na kiwango cha chini cha $600 / mwaka kama klabu ina wanachama 12 au chini. 

 

Taarifa za Kuorodhesha

Taarifa zifuatazo za klabu za shirika zinasambazwa, maofisa wa klabu lazima wahakikishe kuwa ni za hivi karibuni.     

 

taarifa za klabu za kusambazwa
Aina ya Taarifa Zinasambazwa kwa
Jina la klabu, namba, na siku ya kuanzishwa Hadhira
Ratiba ya mkutano Mabalozi wa Agora na maofisa wa shirika la Agora
Mahali pa mkutano Hadhira
Maofisa wa klabu na taarifa zao za mawasiliano Mabalozi wa Agora na maofisa wa shirika la Agora
Muundo wa ada Faragha, haisimamiwi na Agora Speakers International
Fedha za klabu       Faragha, haisimamiwi na Agora Speakers International
Vizuizi vya kutembelewa Hadhira
Vizuizi vya Maudhui ya Hotuba Hadhira
Taarifa za mawasiliano za klabu Hadhira
Tuzo na Medali Hadhira
Lugha za klabu Hadhira
   

 

Uangalizi wa Muundo wa Kielimu wa Agora

Klabu za shirika zina uhuru mwingi wa kutengeneza mpango wetu kukidhi mahitaji yao. Kama ukiombwa, tunaweza tukatoa Mpango wa Kielimu uliorekebishwa ambao unajumuisha mada ambazo zinawavutia na miongozo ambayo inakusanyisha mada zetu za kufunza na mada ambazo shirika linahitaji.

Mikutano ndani ya klabu za shirika inaweza ikawa na vipengele ambavyo havipimwi muda au kutathminiwa (japokuwa hatupendekezi hivyo).

Kuhusu hotuba, klabu za shirika zinaruhusiwa kuweka vizuizi zaidi kwenye maudhui ya hotuba ili vilingane vyema na malengo ya biashara ya shirika. Hawana vigezo vya kuwa shughuli, hotuba, au majukumu lazima yatoke kwenye katalogi ya kawaida.

Kwa nyongeza, klabu za shirika zina uhuru wa kuandaa Mwaka wao wa Kielimu jinsi wanavyoona inafaa - bila kuhitaji kufikia kiwango cha chini cha miaka cha shughuli tofauti (kwa mfano, klabu ya shirika inaweza isiwe na midahalo yoyote au kongamano mwaka mzima kama hawadhani kuwa aina hiyo ya shughuli ni muhimu). 

Mwisho, klabu za shirika hazina ulazima wa kuwa na maofisa wote ambao wamepigiwa kura na wanachama - baadhi ya maofisa wanaweza wakachaguliwa na shirika linaloandaa. Baadhi ya maofisa pia wanakuwa sio wa lazima:

  • Makamu wa Rais wa Uongozi wa Jamii
  • Mweka Hazina
  • Msimamizi wa Jamii

Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:44 CEST by agora.