Loading...
 

Klabu zenye Vizuizi

Uanachama

Kama jina linavyodhihirisha, klabu zenye vizuizi ni klabu ambazo watu ambao wana vigezo fulani tu ndio wanaruhusiwa kuwa wanachama. Vigezo hivi kwa kawaida ni vya aina mbili: 

  • Kitaaluma - ni klabu inayoruhusu wanachama wa shirika la kitaaluma.
  • Kielimu - ni klabu inayoruhusu wanachama ambayo wamefikia kiwango flani cha elimu au mafanikio ya kitaalam.

Vigezo hivi lazima viwe wazi na visiwe dhidi ya kanuni za msingi au sheria za shirika.

Kwa ujumla, kizuizi kinazingatiwa kuwa sahihifu kama mtu yoyote, bila kujali hali yake, anaweza kukizangatia kwa juhudi na utashi wake mwenyewe.

Kwa mfano, kuhitaji uanachama katika shirika maalum au harakati unaruhusiwa kama tu shirika hilo halibagui: Agora inazingatia, hamna tofauti yoyote kati ya klabu ambayo ni ya wanaume tu na klabu ambayo inahitaji wanachama kuwa kwenye shirika ambalo linakubali tu wanaume. Zote zinazingatiwa kuwa za ubaguzi na haziruhusiwi.                                                     

Hii hapa ni baadhi ya mifano ya vizuizi vilivyo sahihi na visivyo sahihi. Kwa vizuizi ambayo sio sahihi, sababu imeelezea.

  • Ni kwa ajili ya madaktari tu
  • Ni kwa ajili ya mawakili tu
  • Ni kwa ajili ya wanachama wa Boy Scout tu (ukiachana na jina, Boy Scouts of America inakubali wasichana pia tangu 2018)
  • Ni kwa ajili ya wanachama wa Mensa tu
  • Ni kwa ajili ya wanaume tu    (ina ubaguzi wa kijinsia)     
  • Ni kwa ajili ya wanawake tu (ina ubaguzi wa kijinsia)     
  • Ni kwa ajili ya Wahispania tu  (ina ubaguzi wa kitaifa)
  • Ni kwa ajili ya Wakristo tu (ina ubaguzi wa kidini)
  • Ni kwa ajili ya wasimamizi wa miradi waliohakikiwa na PMP tu
  • Ni kwa ajili ya wanachama wa IEEE tu
  • Ni kwa ajili ya wanafizikia tu
  • Ni kwa ajili ya wanachama waliomaliza Mpango wa Msingi wa Elimu tu
  • Ni kwa ajili ya wazungumzaji wakitaalam tu
  • Ni kwa ajili ya wanachama wa Chama cha Ujamaa tu (ina ubaguzi wa kiitikadi)
  • Ni kwa ajili ya wanajimu wakitaalam tu (ni dhidi ya sheria ndogo - inaipa umaarufu sayansi na umakinifu)
  • Ni kwa ajili ya watu wenye wapenzi wa jinsia tofauti na yao tu (ina ubaguzi wa chaguo la wapenzi/kimwili)
  • Ni kwa ajili ya Wamama tu (ina ubaguzi wa kijinsia)

 

Kumbuka kuwa usahihifu au la wa kizuizi kinaweza kuwa ni cha nchi maalum.

Kwa mfano, kama nchi inaruhusu wanawake na wanaume wote wawe mawakili, klabu ya wakali tu ni sahihi. Lakini, kama ni wanaume tu ndio wanaweza kuwa mawakili, klabu ya mawakili tu haitoruhusiwa.

Vizuizi vya Umri

Kama kwenye suala la Klabu za Umma, Klabu zenye Vizuizi zinaweza kuwa na kizuizi vya umri sawa na vizuizi viliyoelezewa kwenye Klabu za Umma za Vijana.

 

Mahali pa Mkutano

Klabu zenye vizuizi zina uhuru wa kuchagua mahali popote wanapotaka kwa ajili ya mkutano, lakini isiwe tu ni safu ya nyongeza ya ubaguzi kwa wanachama.

 

Wageni na Wanaozuru

Klabu zenye vizuizi lazima zikubali kutembelewa japo na makundi haya yafuatayo:

  • Maofisa wa Shirika la Agora Speakers International na wanachama wa Bodi ya Wakurugenzi wa Agora Speakers International (kwa ajili ya ukaguzi, uadilifu, ukurufunzi/ushauri)
  • Mabalozi wa Agora
Klabu zenye vizuizi kutembelewa na kundi la hapo juu haimaanishi kuwa wanaruhusiwa kufanya majukumuu yoyote wanayotaka. Ni chaguo la klabu kuwapa majukumu ya kufanya wakati wa mkutano wa klabu. 

Pendekezo letu ni ifuatavyo:

  • Mabalozi wa Agora: Utathmini, Majukumu ya uongozi wa vipengele (kwa mfano, Msimamizi wa mdahalo, Kiongozi wa Hotuba za Papohapo, nk.), na warsha

Tofauti na klabu za umma, klabu zenye vizuizi sio lazima (wanaweza kufanya wakitaka) kukubali wageni kutoka klabu zingine au umma wa kawaida, haijalishi kama wana vigezo vya uanachama.

Vigezo vya Kifedha

Kuhusu fedha, klabu zenye vizuizi zinatakiwa kufuata masharti sawa kama Klabu za Umma.

Lakini, tofauti na klabu za umma, klabu zenye vizuizi zinalipa Agora Speakers International ada ya $40 kwa kila mwanachama kila mwaka. Ada hii inalipwa kwenye siku ya kujiunga ya mwanachama na ni kwa mwaka mmoja.

 

Taarifa za Kuorodhesha

Taarifa zifuatazo za klabu zenye vizuizi zinasambazwa, na lazima maofisa wa klabu wahakikishe ni za hivi karibuni.

 

taarifa za klabu za kusambazwa
Aina ya Taarifa Zinasambazwa kwa
Jina la klabu, namba, na siku ya kuanzishwa Hadhira
Ratiba ya mkutano Mabalozi wa Agora na maofisa wa shirika la Agora
Mahali pa mkutano Hadhira
Maofisa wa klabu na taarifa zao za mawasiliano Mabalozi wa Agora na maofisa wa shirika la Agora
Muundo wa ada Hadhira
Fedha za klabu Wanachama wa Agora
Vizuizi vya Kutembelewa Hadhira
Vizuizi vya Maudhui ya Hotuba Hadhira
Taarifa za mawasiliano za klabu Hadhira
Tuzo na Medali Hadhira
Lugha za Klabu Hadhira
   

 

Uangalizi wa Muundo wa Kielimu wa Agora

Kuhusu suala uangalizi wa Muundo wa Kielimu wa Agora, klabu zenye vizuizi zinatakiwa kufuata masharti sawa kama Klabu za Umma, isipokuwa ya hivi vifuatavyo:

  • Zaidi ya vizuizi vya hotuba vya kawaida ambavyo klabu ya umma zimeweka, klabu zenye vizuizi wanaweza wakaweka vizuizi vya hotuba kuwa ni mada zinazowavutia/wanazozipenda wanachama kwasababu vizuizi hivi vinahusiana dhahiri na vizuizi vya uanachama.
  • Inaruhusiwa kutangaza asasi au mashirika ya kitaaluma ambayo yanakuwa kama kigezo cha uanachama. Kwa mfano, kama klabu ni ya wataalam wa IT (teknolojia ya habari na mawasiliano) tu ambao ni wa ACM, ni sawa kuitangaza ACM ndani ya klabu.

 


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:43 CEST by agora.