Loading...
 

Maudhui ya Hotuba

 

Maudhui ya Hotuba - "Ni nini ninaweza kuzungumzia?"

 

 

Speaker19

 

Ndani ya klabu, unaweza  a club, unaweza kuzungumzia chochote unachokipenda ambacho kipo kwenye mipaka ifuatayo:

  • Hotuba zote zinabidi zitii sheria za mahali maalum. Kwa mikutano ya mtandaoni, mamlaka itakayofuata ni wapi klabu imeandikishwa rasmi.
     
  • Kwa Njia za Kielimu, mada za hotuba zinaweza zisiwe kuhusu uzungumzaji mbele ya hadhira. (Kwa mfano, unaweza usichague "jinsi ya kutumia Utofauti wa Sauti" kama mada ya hotuba yako kwenye mradi wa Utofauti wa Sauti). Unahitaji kizuizi hiki ili uweze kujifunza jinsi ya kutumia mbinu tofauti ili kuongezea hotuba yako, na sio mwisho wenyewe. Kizuizi hiki hakihusiki kwenye hotuba zinazowasilishwa kwenye vipengele vingine vya mikutano.
     
  • Hotuba za chuki haziruhusiwi. Tunatumia maana ya hotuba za chuki ya Umoja wa Mataifa. Hususan:  "Hotuba ya chuki ni mawasiliano yoyote ndani ya hotuba, maandiko au tabia, ambayo yanashambulia au yanayotumia lugha ya dharau au ubaguzi dhidi ya mtu mmoja au kundi la watu kwasababu ya wao ni wakina nani, kwa maneno mengine, kutokana na dini, kabila, utaifa, asili, rangi, uzao, jinsia au utambulisho mwingine. Hii inajumuisha hotuba ambazo zinaanzisha au kuchochea vurugu, ubaguzi, uhasama, au unyama wowote dhidi ya makundi ya watu".

    Tafadhali tambua kuwa vichekesho, ukosoaji, au kuwa "kukwaza" tu kwa mtu haizingatiwi kuwa hotuba ya chuki na haijazuiliwa na sehemu hii.

     
  • Vizuizi vilivyotambulishwa na vilabu.
    • Kila klabu inaweza ikazuiza aina ya mada zinazoruhusiwa kwenye hotuba, maadam vizuizi ni vya kawaida na hazikiuki kanuni kuu za Kutokuwamo na Uaminifu wa Weledi.
    • Vizuizi vinaweza kuelezewa aidha kama seti ya mada zilizozuiliwa au kama seti ya mada za lazima (haswa kwa klabu za kitaaluma, shirika, au manufaa-maalum)
    • Vizuizi lazima viwe na vielezo/bila upendeleo.
    • Vizuizi havitakiwi kwenda dhidi ya mada zozote za malengo ya Taasisi kama sheria ndogo zetu.
    • Hii hapa ni mifano ya vizuizi vya halali:

       

      • Hamna hotuba kuhusu Dini
      • Hamna hotuba kuhusu Mpira
      • Hamna hotuba kuhusu Siasa
      • Hamna hotuba kuhusu Watu Maarufu
      • Hamna hotuba kuhusu Kujamiiana au Kutaka Kujamiiana
      • Hamna hotuba kuhusu kuuza bidhaa au huduma.
      • Hamna hotuba za kujitangaza kibinafsi.
      • Hotuba za kuhusu Historia tu
      • Hotuba kuhusu Dini tu (kumbuka: kizuizi hiki lazima kiruhusu hotuba ambazo zinazungumzia kutokuwepo kwa dini, kama vile uagnosti au uatheisti(kukana Mungu))
      • Hotuba kuhusu Sayansi na Teknolojia tu
      • Hotuba kuhusu Kusafiri tu
      • Hotuba zenye majadiliano ya kisheria tu.
      • Hotuba kuhusu mauzo tu
      • Hotuba kuhusu mambo yanayohusiana na kazi tu (kwa kawaida kwenye klabu za shirika)
         
    • Hii hapa ni baadhi ya mifano ya vizuizi visivyo halali na sababu kwanini sio halali:

       

      • Hotuba za kujisikia vizuri tu (Inategemea)
      • Hamna hotuba za kukwaza (Inategemea)
      • Hamna hotuba zinazovuruga hali nzuri ya klabu (Inategemea)
      • Hamna hotuba za kuwekea mashaka dhidi ya Sayansi (Inapinga sheria)
      • Hamna hotuba kuhusu Uislamu (Haina kutokuwamo)
      • Hamna hotuba kuhusu Ujamaa (Haina kutokuwamo)
      • Hamna hotuba za kukosoa serikali (Haina kutokuwamo)
      • Hotuba kuhusu Chama cha Ujamaa tu (Haina kutokuwamo)
      • Hamna hotuna kuhusu Mageuzi ya binadamu (Inapinga sheria)
      • Hamna hotuba za Sayansi ya Jadi (Inapinga sheria)
      • Hamna hotuba kuhusu Sayansi ya Bandia (Haina kutokuwamo)
      • Hamna hotuba kuhusu bidhaa za mshindani wetu (Haina kutokuwamo)
      • Hamna hotuba kuhuzu Unazi (Haina kutokuwamo)
      • Hotuba kuhusu "Homeopathy" (mfumo wa kutibu magonjwa kwa kutumia kiasi kidogo cha madawa)(Inapinga sheria)
      • Hotuba kuhusu Ukristo tu (Haina kutokuwamo)
      • Hotuba kuhusu Sayansi isiyo rasmi tu (Inapinga sheria)
      • Hotuba kuhusu madawa yasiyo ya jadi (Inapinga sheria)
         
    • Tuseme klabu imechagua kuzuia mada za hotuba. Kwenye suala hili, vizuizi lazima vitangazwe kwa umma na viwe wazi kwenye sehemu zote ambazo klabu zina uwepo mtandaoni (tovuti, kundi la Facebook, nk). Lazima ielekeze dhahiri vizuizi hivyo kwa wageni na wanachama watarajiwa.
       
    • Wanachama lazima wapige kuwa mabadiliko ya vizuizi.
       
  • Mwisho, kumbuka kuwa baadhi ya miradi (haswa kwenye Njia ya Juu ya Kielimu) au shughuli (kama Mashindano) vinaweza kuweka vizuizi vya aina gani za hotuba zinazokubaliwa au hata kuhitaji uandike kuhusu mada fulani maalum.
     
  • Hotuba za nje ya klabu (kwa mfano, ambazo zinatolewa kwenye Mikutano, nk.) zinaweza kuwa na vizuizi vingine vya ziada.

 

Kama kuna mashaka yoyote, jisikie huru kututumia ujumbe kwenda info at agoraspeakers.org.

Je, inakuwaje kama sijafurahishwa na vizuizi vilivyowekwa na klabu?

Kama haufurahishwi na vizuizi kwenye klabu yako, una machaguo matatu:

  • Kama unaamini kuwa vizuizi vinakiuka masharti ya Agora Speakers International, tafadhali jaribu kusuluhisha ndani ya chama kwanza kwa kuwashughulisha maofisa wa klabu na kuwaonyesha ukurasa huu. Kama suala hili haliwezi kusuluhishwa, tafadhali tutumie kiunganishi au nakala ya vizuizi vya hotuba ya klabu kwenda info at agoraspeakers.org, ukielezea kwanini unaamini kuwa zinakiuka masharti yaliyowekwa. Tafadhali weka pia jina la klabu na namba.
     
  • Unaweza ukapendekeza mabadiliko na kuweka pendekezo maalum mbele ya wanachama wa klabu yako kwa ajili ya kupiga kura.
     
  • Daima unaweza ukaanzisha klabu mpya ambayo haina vizuizi hivyo.

 

 


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:29 CEST by agora.