Loading...
 

Dhamira Yetu

 

Dhumuni Letu

 

Agora Speakers International ni shirika lisilo la kibiashara lenye watu wenye shauku ya kujitolea kuwasaidia watu kujiendeleza kwenye uzungumzaji wa mbele ya hadhira, mawasiliano, umakinifu, debating, na ujuzi wa uongozi.

Dhamira Yetu

Agora inakuwezesha kuwasiliana vizuri na kuwa kiongozi anayejiamini ambaye atajenga dunia iliyo bora.

 

Kufunza Ujuzi laini

Tunasaidia watu kuendeleza seti za msingi za ujuzi ambazo zinahusu Uongozi:

Skills

 

Baadhi ya ujuzi ambao utajifunza na kujiendeleza ndani ya Agora: 

kufunza ujuzi laini
Ujuzi wa Mawasiliano
Uzungumzaji wa Mbele ya Hadhira Uandishi wa Hotuba Utajiri wa Lugha Lugha za Kigeni Mawasiliano yasiyo ya maneno
Kuadithia hadithi Uwasilishaji Uwepo wa jukwaani Mawasiliano ya Kuona Uwazi wa Lugha
         
Ujuzi wa Uongozi
Maoni ya Kujenga Ukufunzi Dira Uzingatiaji na Fokasi Ushawishi
Kuchukua hatari Utambuzi Maafikiano Kuhamasisha wengine Kuwa kocha
         
Umakinifu
Majadiliano Kujenga hoja Utafiti Uaminifu wa Weledi Uchambuzi wa Tatizo
Maarifa ya kisayansi Udadisi Kufikiri kimantiki Ubunifu Unyumbufu wa Tambuzi
         
Ujuzi kati ya watu
Hisia-mwenzi Usikilizaji Maarifa ya Kijamii Hisia Huruma
Usimamizi wa Mahusiano Upatanisho Kujenga Mahusiano    
         
Ujuzi wa Tabia Binafsi
Kujiamini Kujithibiti Uvumilivu Kutegemewa Kuwa chanya
Ustahimilivu Msimamo wa Kutegemea Mazuri Uaminifu Kuwa kwenye wakati Utathabiti
Ujasiri Unyenyekevu Ushupavu    
         
         
Ujuzi wa Usimamizi
Kuratibu na Kuandaa Kukabidhi kazi Utathmini wa Hatari Usimamizi wa Hatari Uchangishaji fedha
Usimamizi wa Muda Usimamizi wa Bajeti Masoko Uhusiano wa Umma Kupanga malengo na ufatiliaji
Kuandaa Matukio Ujasiriamali Kufikiria kimkakati Usimamizi wa Mabadiliko Kuajiri
         
         
Kufanya kazi kama timu na ujenzi wa timu
Ukufunzi Kufundisha Kusuluhisha Ugomvi Uratibu wa Timu Timu zenye tamaduni tofauti
Kufahamu utofauti Kujenga mtandao Uwezo wa mchanganyiko wa tamaduni Kushirikiana Kujumuisha

 

Nitapata nini?

Kujiunga Agora Speakers International kutakupa faida nyingi sana kwenye viwango vyote, katika maisha ya kibinafsi na kitaaluma. 

Hizi ni baadhi ya faida ambazo utapata utakapojiunga na Shirika letu:

  • Utajifunza kuwasiliana kwa ufanisi zaidi
  • Utajifunza kutumia zana za aina zote kama vile hadithi, visa vya kusisimua, ucheshi, na hisia ili kuziruhusu hotuba zako kuwa za kitofauti na kuwa na matokeo.
  • Utajifunza kuhamasisha watu kutenda na kuongoza timu ndogo na kubwa.
  • Utaongeza kujiamini kwako, uthubutu wako na uwezo wa kutetea yale unayoyapenda.
  • Utajifunza jinsi ya kukabiliana na kufeli na kufikiria haraka haraka, na jinsi ya kutenda pale ambapo vitu visipoenda kama vilivyotarajiwa.
  • Utakuwa unaweza kufikiria kimantiki, na utaweza kugundua kirahisi pale mtu atakapokuwa anakurubuni kufanya maamuzi ambayo ni tofauti na kile unachokitaka.
  • Utakuwa mwanachama wa ulimwengu mzuri, wenye msaada, na jamii iliyo karibu.
  • Utaweza kupata seti za huduma ambazo zinaendelea kukua.
  • Utapata uwezo wa kutetea mitazamo na kanuni zako
  • Utakuwa msikilizaji mzuri na anayejali hisia za wengine
  • Utaweza kuacha matokeo chanya na ya muda mrefu kwenye jamii yako na duniani kwa ujumla. 

 

Inakuwaje kama sizungumzi mbele ya hadhira?

Ni dhana potofu kuwa mbinu za uzungumzaji wa mbele ya hadhira na mafunzo ni muhimu tu wakati unazungumza mbele ya hadhira. Kiuhalisia, huo sio ukweli kabisa. Unapoendelea kwenye mpango wetu, utaona kuwa mtindo wako wa mawasiliano una maendeleo hata kwenye mazungumzo na mtu mmoja, sio tu kwenye kitaaluma lakini pia kibinafsi. Utaweza kuelezea mawazo yake vizuri zaidi, kusikiliza wengine, kugundua uongo na masuala kweye hoja zao, kufikia mapatano, na kwa ujumla kuwa na hotuba yenye utajiri na ya kushawishi zaidi.

 

Ujunzi ambao tunafundisha na kufunza…

  • …kuwezesha watu kufuatilia ndoto zao za kitaaluma na kibinafsi.
  • …kuunda viongozi ambao wana matokeo chanya kwenye mazingira yao.
  • …kuunda wananchi wenye taarifa zaidi ambao hawawezi kudanganywa, matokeo yake ni jamii imara na yenye afya.

Utaona maendeleo kwenye namna ambayo unawasiliana na watu kwenye nyanja zote za maisha yako, na muhimu zaidi - utaanza kupata matokeo. Cha zaidi - matokeo hayo yatakuja haraka. Ukiwekeza japo muda wa kutosha kuhudhuria na kushiriki kwenye mikutano ya klabu japo mara mbili kwa mwezi, utashangaa maendeleo yako ndani ya miezi 3-4. 

 

Kwanini hii ni muhimu?

Ujuzi laini ambao tunakusaidia kuboresha ni muhimu kwenye maendeleo ya kazini na maisha kwa ujumla, na kuna tafiti nyingi sana zinazosaidia matamko haya:

  • Ndani ya "Ushahidi mgumu kwenye Ujuzi Laini", Heckman na Kautz walionyesha kuwa elementi nyingi za maisha yako ya kitaaluma na binafsi zinahusiana moja kwa moja na uwezo wako wa ujuzi laini. Kwa maneno mengine, "ujuzi laini unatabiri mafanikio kwenye maisha."
  • Waajiri wanaorodhesha sana ujuzi laini (na, hususan, ujuzi wa mawasiliano) kama ujuzi wa juu wanaovutiwa nao sana kwenye watu wanaotafuta kazi.
  • Kwenye tafiti moja maalum iliyofanywa na Indeed.com, ujuzi mbili ambazo waajiri wanaangalia sana ni Mawasiliano na Uongozi.
  • Kulingana na tafiti iliyofanywa na American Journal of Psychiatry, uoga za kuzungumza mbele ya hadhira, ni aina ya wasiwasi wa kijamii:
    • Inapunguza uwezekano wako wa kumaliza chuo kwa mafanikio kwa 10%
    • Inapunguza mshahara wako kwa 10%
    • Inapunguza uwezekano wa kazi ya kiufundi, kitaaluma, au usimamizi kwa 14%.
  • Haupo pekee yako - Uzungumzaji wa mbele ya Hadhira ni sababu kubwa ya wasiwasi wa kijamii na hofu ya kijamii, kwa 89.4%.

 

Mimi sio kiongozi!

Unaweza kufikiria kuwa wewe sio kiongozi "wa kuzaliwa". Kuwa hauna "kile kinachotakiwa". Kuwa daima umekuwa una haya na kamwe haujawahi kushawishi chochote.

Basi, utashangaa kuwa viongozi wengi, kwa uhalisia, ni kama wewe.

Viongozi wanatengenezwa, hawazaliwi. Na hili sio tu wazo - kuna utafiti unaoongezeka kuwa uongozi ni kitu ambacho kinaweza kufundishwa na kufunzwa.

Sio tu kwasababu viongozi wanatengenezwa na sio kuzaliwa inamaanisha kwamba uongozi ni rahisi na nyoofu. Inahitaji juhudi, utashi, na nidhamu. Lazima uwe na nia ya kuwekeza muda wako, kuendelea na bila kukata tamaa kusukuma mipaka ya eneo ambao umelizoea, na usiache pale utakapokumbana na kikwazo cha kwanza.

Uongozi pia unaweza kuwa wa umbo tofauti:

  • Unaweza kuwa kiongozi kupitia ujuzi wako wa biashara, kama vile Jeff Bezos au Jack Ma.
  • Unaweza kuwa kiongoz kupitia uwezo mkubwa wa kiakili, kama vile Albert Einstein, Sam Harris,  Jordan Peterson, au  Neil DeGrasse Tyson.
  • Unaweza kuwa kiongozi kupitia kazi yako, kama vile Thomas A. Edison
  • Unaweza kuwa kiongozi kupitia haiba yako, kama vile John F. Kennedy
  • Unaweza kuwa kiongozi kupitia kujitolea kwako, kama vile Nelson Mandela
  • Unaweza kuwa kiongozi kupitia uthabiti wa msimamo wako na kujitoa kwa kanuni zako, kama vile Papa John Paul II au Mahatma Gandhi.
  • Unaweza kuwa kiongozi kupitia huruma, kama vile Mama Theresa wa Calcutta au Lady Diana, Binti Mfalme wa Wales.
  • Unaweza kuwa kiongozi kupitia hisia kali na msimamo, kama Martin Luther King.
  • Unaweza kuwa kiongozi kwa kusimamia haki zako, kama vile Rosa Parks au Greta Thunberg.
  • Na pia, unaweza kuwa kiongozi kupitia jeshi, kama vile Napoleon Bonaparte, ingawa tungependelea utumie ujuzi huo kwenye kutatua matatizo kwa amani. 
Hauhitaji kuwa na "tabia (sifa) za uongozi" zote. Kuna njia nyingi za uongozi. 

 

Je unataka kuzungumza kama Ronald Reagan au Barack Obama? Kuongoza kama Martin Luther King?

Kama ni hivyo, tuna habari nzuri na mbaya kwa ajili yako. Habari mbaya ni kuwa hauwezi kuzungumza kama Ronald Reagan. Kulikuwa na Ronald Reagan mmoja tu kwenye historia, na hauwezi kuwa yeye. Pole. Hauwezi kuwa Barack Obama, aidha. Au mzungumzaji au kiongozi yoyote maarufu. Na hiyo ni vizuri kwasababu fikiria jinsia gani dunia ingechosha na kuwa hafifu kama wazungumzaji wa mbele ya hadhira wangezungumza kama mhutubu wa Kiromani Marcus Tullius Cicero. Badala ya Lincoln, Churchill, Reagan, Obama, Luther King, na wengine wengi, tungekuwa na watu wengi kama Cicero.

Habari nzuri ni kuwa unaweza kuwa wewe mwenyewe. Hakujawahi kuwa na mtu kama wewe kwenye historia ya dunia, na hakuwezi kuwa na mwingine. Unaweza kuunda mtindo wako mwenyewe wa kuzungumza mbele ya hadhira na uongozi, kutokana na jinsi ulivyo, kwa haiba yako mwenyewe. Na hiko ndicho kitakufanya kuwa wa kipekee.

Ndani ya Agora, tunaweka msisitizo kwenye kutafuta na kuendeleza mtindo wako mwenye kuliko kujaribu kumuiga mtu mwingine. Utajifunza mitindo mingi ya uzungumzaji na uongozi, utapata mawazo na mbinu ambazo unazipenda. Utajifunza kuhusu zana za msingi za balagha, majadiliano, usimamizi, ushawishi. Na ukiwa na vipande vyote hivi, utajenga mtindo wako mwenyewe wa kipekee.

 

Siwezi kufanya mabadiliko!

Dunia ipo katika hali mbaya mpaka unafikiri kuwa hauwezi kufanya mabadiliko. Matatizo ni makubwa sana na yanaonekana hayawezi kutatuliwa. Kuna ukandamizaji, ugomvi, mabadiliko ya tabia ya nchi, umaskini, ubaguzi, vita. Je mtu yoyote anawezaje kufanya mabadiliko, haswa kama hawana nguvu (mamlaka), maarifa, ushawishi, au ujuzi?

Lakini, hauhitaji kupata masuluhisho ya matatizo ya dunia. Unahitaji tu kusuluhisha tatizo moja dogo kwa ajili ya mtu ili kufanya mabadiliko.

Na mara nyingine, kwa kuanza tu kufanyia kazi tatizo na sio tu kuliongelea, utapitia kitu tofauti cha kustaajabisha.

 

Starfish

Mrusha Nyota
(imefupishwa na kutoholewa kutoka hadithi halisi iliyoandikwa na Loren Eiseley)

Bahari za Costabel zimejaa takataka za uchafu wa maisha. Koe zinatupwa kwenye upepo; kaa mpweke, akitafuta nyumba mpya kwenye kina, ametoswa kwenye ufukwe, ambapo shakwe zinamkata vipande vipande.

Mbele yangu, upinde mkubwa wa mvua mzuri unaomeremeta umeibuka. Mahali fulani kuelekea kwenye mguu wa upinde wa mvua, nilimuona binadamu amesimama, alionekana kwangu, ndani ya upinde wa mvua, japokuwa hakufahamu nafasi yake. Alikuwa anaangalia kitu kwa umakini kwenye mchanga. 

Mwishowe, aliinama na kutupa kile kitu kwenye mawimbi. Nilitembea kumfuata kwa takriban nusu maili nikitembea bila uhakika. 

Wakati namfikia, upinde wa mvua ulikuwa umefifia mbele yetu, lakini kitu kwenye rangi zake ulikimbia haraka kwenye umbo lake. Alikuwa anaanza kupiga magoti tena.

Kwenye bwawa la mchanga na mchangatope, samaki wa aina nyota alikuwa amenyonya mikono yake kiukakamavu na alikuwa ameshika mwili wake kutoka kwenye matope magumu.

"Bado yupo hai," Nilisogea.

"Ndio," alisema, na kwa mwenendo mwepesi lakini wa haraka, alinyanyua nyota na kuirusha mbali kwenye bahari. Ikazama kwenye mawimbi, na maji yakaunguruma tena.

"Anaweza kuishi," alisema, "kama mvuto wa fukwe una nguvu ya kutosha." Aliongea kwa utulivu, na usoni mwake, mwango bado ulikuja na kuondoka kwa rangi tofauti.

"Hamna wengi ambao wanaokuja umbali huu," nilisema, nikapata aibu ya maneno ghafla. "Je unakusanya?"

"Kwa namna hii tu," alisema kwa utaratibu, akionyesha ishara ya mabaki ya ufukwe. "Na kwa ambao wapo hai tu." Akainama tena, na mimi kwa kutaka kudadisi, nikarusha nyota nyingine kwenye maji.

"Nyota," alisema, "rusha vizuri. Mmoja anaweza kuwasaidia."

"Kuna nyota nyingi sana ambazo zinakufa kwenye bahari. Uokoaji wa nyota moja italeta mabadiliko gani?"

"Kwa nyota ile, imefanya mabadiliko makubwa."

Nikageuka nilivyofikia upindo wa bahari na nikamuona anarusha nyota nyingine, akiirusha kwa ustadi mkubwa sana kwenye maji. Kwa muda mfupi, kwenye mwanga unaobadilika, alionekana amekuzwa, kama vile anarusha nyota kubwa kwenye bahari kubwa zaidi. Alikuwa, katika kiwango chochote, na mkao wa mungu.

(...)

Kwenye sehemu nchi kavu, kama vile anajitokeza kwenye makao zaidi yetu, nilimpata mrusha nyota. Kwenye asubuhi yenye harufi nzuri ya mvua, upinde wa mvua wenye rangi nyingi bado ulionekana na ukawa unayumba mbele yake. Kwa ukimya nilitafuta na nikanyanyua nyota ambayo bado ilikuwa ipo hai, ambaye mirija ya miguu yake ilikaa kwenye vidole vyangu wakati, kama nyota ya kweli, kikalia bila sauti kwa maisha yake. Nilimuona kwa uwazi zaidi na nikamtupa mbali zaidi, akazunguka mbali zaidi kwenye mawimbi. Nikazungumza mara moja kwa ufupi. "Naelewa," nilisema. "Niitie mrushaji mwingine." Na hapo tu ndio nikajiruhusu kufikiria. Hayupo pekee yake tena. Baada yetu, kutakuwa na wengine.

Inataka ujasiri kuchukua nyota ya kwanza na kuitupa baharini chini ya macho ya watu. Inaweza kuonekana kama haina maana, lakini sio tu kuwa umefanya mabadiliko makubwa kwa nyota yule - umeweka mfano kwa wengine. Umeshinda vikwazo vya kiakili ambavyo vinakuambia kuwa "hamna kitu unachokifanya ambacho kitakuwa na umuhimu," na umebadilisha kutokujali kuwa matendo. Mara utakapochukua hatua ya kwanza, wengine ambao wameona mfano wako watafuata. Wanaweza wasijiunge hapo hapo, haswa kwasababu watu wengi wanakata tamaa kiurahisi sana baada ya kikwazo kimoja na hivyo tumejifunza kuwa na mashaka. Lakini kama ukiendelea, kama umejishawishi kuwa kile unachokifanya kina maana, wengine watajiunga pia. Mpira huu mdogo ambao umekuwa ukiusukuma utakuwa mkubwa na mkubwa, ukikusanya kasi na usaidizi mpaka utakapokuwa wimbi la mabadiliko lisiloweza kuzuilika.

Na hii sio tu hadithi ya kuhamasisha ya kujisikia vizuri. Inatokea mara nyingi sana katika maisha ya kila siku. Lakini wewe lazima uchukue hatua ya kwanza, unaamini kwenye kile unachokitaka kukifanya, na lazima uendelee.

 

Mabadiliko ya ufukwe wa Versova - kabla na baada
Mabadiliko ya ufukwe wa Versova - kabla na baada

Mabadiliko ya ufukwe wa Versova mjini Mumbai
(kutoka kwenye ripoti halisi kutoka CNN)


"Nilihamia kwenye fleti yangu miaka miwili nyuma na kuona plastiki kwenye bahari – zilikuwa na urefu wa futi 5.5. Mtu angeweza kuzama kwenye plastiki," Shah aliwaambia CNN. "Nikasema nitanya kitu. Inabidi nilinde mazingira yangu, na inahitaji matendo."

Shah, 33, alianza kusafisha bahari mwaka 2015 akisaidiwa na jirani. Baada ya muda, watu 1000 walijitolea kumsaidia, ikiwemo watu waliokuwa wanaishi Versova pia, watu wasio na makazi, wanasiasa, watu mashuhuri wa Bollywood, na watoto wa shule.

Watu waliojitolea walisafisha pia vyoo vya umma 52 vilivyopo kwenye fukwe na walipanda minazi 50. Shah anasema anataka kupanda minazi 5,000 na kupabadilisha kuwa "wangwa la minazi kama ilivyokuwa hapo kabla."

Katika kipindi cha miezi 21, watu waliojitolea wakiongozwa na Afroz Shah walikusanya takataka za kuoza na plastiki takriban kilo millioni 5.3 kutoka kwenye urefu wa kilomita 2.5 wa ufukwe wa bahari.

Umoja wa Mataifa umeipa jina la "mradi mkubwa duniani wa usafishaji", mabadiliko makubwa ya Versova kutoka uchafu kupitiliza mpaka umaridadi umelipuka mtandaoni nchini India, ambapo watu mtandaoni wanasifia watu waliojitolea kwenye usaidizi wao kwenye juhudi hizi kubwa.

 

Ni nini tunakipata?

Aina ya ujuzi laini ambao Agora inatoa kwa kawaida unagharimu maelfu na maelfu ya dola kwenye semina za kitaaluma. Tunatoa bure kutumia mfumo uliothibitishwa - na ambao unaweza kufurahia. Kufikia hapa, utakuwa unafikiria - "basi, ni nini ambacho Agora wanakipata kutoka yote haya?" Sauti ya mashaka ndani ya baadhi ya watu inaweza kusema, "kama haulipii bidhaa, basi wewe ndio bidhaa". Hata hivyo, kuna mifano mingi sana ya bidhaa na huduma bora ambazo unapata bure, ambazo zimetengenezwa na watu waliojitolea wenye shauku ambao wanaamini kwenye jambo, bila data zako kuuzwa au kuchunguzwa, au bila kuchunguzwa ua bila kuhitaji wewe kutoa kitu chochote.

Kama Shirika la Kielimu, tunafurahi kuunda na kujenga viongozi ambao ni wavumilivu, viongozi ambao wana ujasiri, viongozi ambao wanaweza kushawishi kwa maneno yao na sio kwa ugomvi na ukali, viongozi ambao wanasikiliza na kufikiri kimantiki, viongozi ambao hawawezi kurubuniwa kirahisi na viongozi ambao wanaweza kuhamasisha na kufanikisha vitu vikubwa.

Tunafurahi kupambana na janga la sayansi feki ambalo limesababisha maumivu mengi sana, mateso, na kupoteza watu wengi sana.

Tunafurahi kuchangia kwenye jamii zenye amani kwa kuunda na kuunganisha jamii kutoka duniani kote na zenye tamaduni tofauti ambapo watu wanajifunza, wanakuwa, na kuwa na mtandao na wengine kupitia urafiki na uvumilivu.

Tunafurahi kuchangia kwenye uthabiti wa jamii za kidemokrasia kwasababu watu ambao wanafikiria kimantiki na kugundua majadiliano mabaya na data mbaya hawawezi kurubuniwa kirahisi kupigia kura viongozi ambao sio wazuri ambao watakuwa na nguvu nyingi, wataondoa mihimili ya serikali, na kupunguza haki za binadamu za wananchi. Watu ambao wanafikiria kimantiki hawawezi kushawishiwa kuwa kundi lingine la kijamii, asili, dini, au nchi ni chanzo cha matatizo yao na hawatofikiria kuwa ugomvi, uhalifu, au vita ndio suluhisho la tatizo lolote.

Mwisho, tunafurahi zaidi kuwasaidia wanachama wetu kuunda na kuongoza miradi halisi duniani kote, kuifanya sehemu bora zaidi, mradi mmoja, na nyota moja kwa wakati. Kwa ufupi, tunafurahi kuona wanachama wetu wanabadilika kuwa viongozi ambao wanaweza kuzungumza, kuongoza, na kuweka historia.

 

 


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Wednesday July 28, 2021 10:30:12 CEST by zahra.ak.