Loading...
 

Kujiunga na klabu

 

Kama tayari unajua klabu na unataka kujiunga, mwandikie mtu ambaye ameorodheshwa kama pointi ya mawasiliano wa klabu hiyo au Makamu wa Rais, Uanachama (VPM).

Kama hujui klabu yoyote, unaweza:

  1. Angalia kurasa ya nchi yako kama kuna kundi kwenye eneo lako.
  2. Jiunge kwenye kundi la eneo hilo na angalia klabu zipi zinapatikana.
  3. Hudhuria mkutano wao mmoja kama mgeni.
  4. Omba kujiunga!

Kama bado hauwezi kutafuta klabu ya kujiunga, jisikie huru kututumia barua pepe kwenda info at agoraspeakers.org pamoja na mji na nchi yako, na tutajaribu kukuelekeza kwa klabu ambazo tayari zipo kwenye eneo lako.

Ndani ya Agora, unaweza kujiunga kwenye klabu nyingi iwezekanavyo, ili mradi unaweza kushiriki mara kwa mara kwenye mikutano. Na, zaidi ya yote, hauhitaji kulipa kitu chochote kwetu bila kujali kama unataka kujiunga na klabu moja au kumi. Kiukweli, kila klabu inaruhusiwa kutoza ada ya ngongeza za uanachama ili kuweza kulipa gharama za uendeshaji, kama vile kukodi chumba, kuchapisha na kutoa nakala, vifaa vya kusikia/kuona, nk.

Pia, Agora ina Aina za Klabu tofauti ambazo zinatofautiana kwenye kazi zake.

Uanachama wa klabu Club unatakiwa kukubaliwa na klabu. Hata kama wewe ni mwanachama wa Agora Speakers, klabu inaruhusiwa kukataa uanachama wako kwa sababu maalum, zisizo za ubaguzi (kama vile kutokuwepo na nafasi ya kutosha, kutokuwa na baadhi ya vigezo kama vile historia kwenye taaluma maalum, nk.).

Kama unafikiri majibu hasi yalitokana na sababu za kibaguzi (asili, rangi, dini, mvuto wa kijinsia, utambulisho wa kijinsia au unavyojielezea, umri, kiwango cha kipato, utaifa, kabila, au ulemavu wa kiakili au kimwili), tafadhali tutumie ujumbe kwenda info@agoraspeakers.org, na tutafanya uchunguzi zaidi. 

Kama hamna klabu nyingine karibu, unaweza kuanzisha moja! Tunawapa waanzilishi wa klabu usaidizi wa kutosha, mafunzo, na utambuzi wa duniani kote ndani ya jamii yetu. Kama ukianzisha klabu ya kwanza nchini kwako, unaweza pia kuomba kuwa Balozi wa Agora wa Nchi.

 


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:09 CEST by agora.