Loading...
 

Njia ya Juu ya Kielimu

 

Pale Njia ya Msingi ya Kielimu itakapokuwa imemalizika, unaweza kuendelea na Njia ya Juu ya Kielimu yoyote ambayo ipo. Kila njia ya juu ina kati ya vipengele 7 na 15.

Unaweza kufanyia kazi njia zozote za juu kwa wakati mmoja na kuzifanya kwa mpangilio wowote. Unaweza kupumzika kwenye njia moja, na kuanza kufanyia kazi nyingine (au ukapumzika tu kwa ujumla) na kuirudia/kuzirudia baadae utakapokuwa tayari. Kigezo pekee ni kuwa vipengele kwenye kila njia lazima zikamilike kwa mpangilio.

Bila shaka, unaweza kurudia mradi mara nyingi upendavyo, na kiukweli, inapendekezwa kuwa usiendelee mbele kama haujaridhika na matokeo ya mradi uliopita. Haina maana kuwahi mbele ili upate tu beji au tuzo, Kumbuka kuwa lengo kuu ni kusoma, kufanya mazoezi, kujifunza, na kuwa tayari kwa "jukwaa kubwa". Lengo halitakiwi kuwa kukusanya beji. Hamna kikomo cha muda wa kumaliza njia maalum.

Njia za Juu


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:12 CEST by agora.