Loading...
 

Rais

 

 

Rais wa Klabu ni mratibu wa maofisa wote wa klabu, mbunifu wa mikakati ya ujumla ya klabu, na ni mwakilishi wa klabu katika matukio ya nje.

Majukumu ya uongozi ndani ya klabu

Ndani ya Agora, tunatazama nafasi za kiofisa kama nafasi za uongozi kuliko kuwa za usimamizi au ukurugenzi. Kuna tofauti nyingi kwenye

  • Majukumu ambayo ni ya ukurugenzi tu ni ya utekelezaji wa mikakati ya mtu mwingine. Kwa mfano, Makao Makuu ya shirika wanaweza wakaamua kila kitu ambacho kinahitajika kufanyika na kupanga namna ya utekelezaji kwa ofisa, ambaye atatoa ripoti za jinsi utekelezaji unavyoenda kwa makao makuu.
  • Majukumu ambayo ni ya usimamizi yana uhuru kidogo, lakini uongozi wake ni wa uendeshaji tu. Wanaweza wakaunda sheria, kanuni, utaratibu wa uendeshaji, nk. Wanaweza kutengeneza malengo ambayo yanaweza kupimika, kufuatilia maendeleo, nk.
  • Mwishoni, majukumu ya Uongozi zinazingatia picha kubwa zaidi, anatoa dira na kuhamasisha timu yake kutekeleza dira hiyo. Wakati viongozi wazuri wananufaika kama wao pia ni wasimamizi wazuri, sio kigezo kama wanapanga kutoa jukumu hilo kwa mtu mwingine.

 

Uongozi wa utumishi       

Kuna uwepo wa mitindo ya uongozi mingi leo - kutoka Kimamlaka (kiongozi anafanya maamuzi yote) mpaka kimapatano (uongozi unaozingatia utendaji na matokeo) mpaka kiholela (kuachia watu kutambua jambo wao wenyewe). Tutazungumzia kiundani zaidi kwenye Njia wa Uongozi, ambapo tutaona pia kuwa hazina ufanisi sawa.

Kwa Klabu za Agora, mtazamo wetu wa uongozi ni kuwa uongozi bora unafanywa kwa kutoa huduma (utumishi) kwa wengine - kile ambacho nadharia ya uongozi wa kisasa wanakiita "Uongozi wa Utumishi" (japokuwa Robert K. Greenleaf ndiye aliyeliunda neno hilo kwenye miaka ya sabini (1970)):

Uongozi wa utumishi unaonyeshwa kwa kuwezesha na kuendeleza watu, kwa kuonyesha unyenyekevu, uhalisi, kukubali watu, na usimamizi; na kutoa mwelekeo. Mahusiano bora zaidi kati ya watu, uaminifu, na haki zinategemewa kuwa utaratibu wa muhimu sana ili kuhimiza kujitambua, mtazamo chanya wa kazi, utendaji, na uzingatiaji imara wa shirika kwenye uendelevu na majukumu ya kijamii. Dirk van Dierendonck, Chuo Kikuu cha Erasmus - Journal of Management Toleo. 37 Namba. 4, Julai 2011 1228-1261

Uongozi wa utumishi sio tu wazo zuri la maadili: kuna utafiti nyingi zinazohusisha hii na kuongezeka kwa ufanisi wa timu na maendeleo. Angalia, kwa mfano, hapa na hapa.

Ni nini viongozi wazuri wanafanya kwenye mtazamo huu? Mwaka 2008, Robert Linden na washirika wenzake walitambua seti ya vipengele 9 ambazo zinaonyesha kiundani mitindo ya msingi ya uongozi huu:

 

kipengele cha uongozi maudhui
Uponyaji wa kihisia Kitendo cha kuonyesha hisia kwa masuala binafsi ya wengine.
Kuongeza thamani ya jamii Kufahamu na kujali kiukweli kutaka kusaidia jamii
Ujuzi wa dhana Kujua kuhusu shirika na majukumu yaliyopo ili kuweza kutoa msaada kiufanisi na kusaidia wengine, haswa wafuasi wanaokufuata
Kuwezesha Kuhimiza na kuwezesha wengine, wafuasi wanaokufuata, kutambua na kutatua matatizo, na pia kujua lini na jinsi ya kumaliza kufanya kazi
Ukuaji Kusaidia wafanyakazi kukua na kufanikiwa—kuonyesha kujali kiukweli kuhusu ukuaji wa kitaaluma (kazi) na maendeleo kwa kutoa msaada na ushauri
Kuwapa kipaumbele wafanyakazi Kutumia vitendo na maneno kuweka wazi kwa wengine (haswa wafuasi wanaokufuata) kuwa kuridhisha matakwa yao ya kazi ni muhimu (Wasimamizi ambao wanafuata kanuni hii mara nyingi watapumzika kutoka kazi zao ili kusaidia wafanyakazi na matatizo yao ambayo wanapitia kwenye kazi walizopewa.)
Kutenda kimaadili Kushikiana kwa uwazi, kwa haki, na kiukweli na wengine
Mahusiano Kitendo cha kufanya juhudi kiukweli kujua, kuelewa na kutoa msaada kwa wengine ndani ya shirika, msisitizo ukiwa ni kujenga mahusiano ya muda mrefu na wafuasi wanaokufuata
Utumishi Namna ya uainishaji na kutaka kuonekana na wengine kama mtu ambaye anawahudumia wengine kwanza, hata kama kujitolea kunahitajika

(Kutoka "Uongozi wa Utumishi: Maendeleo ya ukadirifu wa kipimo chenye vipengele vingi na viwango vingi",  Linden et al., The Leadership Quarterly Toleo la 19, Namba 2, Aprili 2008)

 

Dira ya Klabu na Mkakati wa Klabu

Kama Rais wa klabu, unatakiwa kuwa na dira (maono) ya wapi unataka kuipeleka klabu na wanachama wake, jinsi unavyowaona kwenye mwisho wa muhula wako wa mwaka mmoja (1), na mkakati gani utatumia kufanikisha hicho. Kuhusiana na hili, Uongozi wa utumishi inahusika haswa kwasababu mkakati unatakiwa kuwa kuhusu klabu yako na wanachama wako: jinsi ya kuwasaidia kukua na kuwa imara. Unatakiwa kuonyesha dira hiyo kwenye tamko la dira ambalo linatoa muhtasari wapi ambapo klabu ipo sasa na ni nini klabu inataka kufanikisha.

Tamko la dira linatakiwa kuwa:

  • Fupi
  • La wazi
  • Kuhamasisha
  • La kutia changamoto
  • Lenye maana kwa wanachama wote

Linaweza kuwa rahisi kama:

Tuna mazingira rafiki na changamfu ya kujifunza kwenye mji wetu.

Wakati unatengeneza tamko la dira, usifikirie tu kuhusu klabu yako kwenye muktadha ya klabu nyingine za Agora (kama vile "tunataka kuwa klabu yenye idadi kubwa ya wazungumzaji wa juu wa mbele ya hadhira" au "tunataka kushinda tuzo nyingi zaidi kwenye mashindano ya Agora"), lakini pia fikiria kuhusu klabu yako kwenye jamii ambayo ipo.

Kumbuka kuwa kiongozi mzuri anahamisha - klabu inatakiwa kuelewa tamko lako la dira.

Tamko la dira na mkakati wa klabu lazima vilingane na malengo na sheria za Agora. Pia, hazitakiwi kupingana na Kanuni zozote za Msingi.

Hamna mkakati wa "saizi moja ya kutosha wote" unaotumiwa na klabu zote. Kila klabu ni tofauti, na mahitaji ya wanachama wake ni tofauti.

 

Mratibu wa Timu ya Maofisa

Kama Mratibu wa Maofisa wa Klabu, unatakiwa kusaidia kutatua matatizo yoyote ambayo yanaweza kujitokeza na kuteua maofisa wa muda mfupi kama ofisa mwenye jukumu hatokuwepo kufanya majukumu yake kwa kipindi kirefu.

Kama ofisa hatokuwepo kwa muda usiozidi miezi miwili (2) wa muhula wake, ni sawa kutafuta mtu mwingine wa kuchukua majukumu hayo au kugawanya majukumu yake kwa maofisa waliobaki. Lakini, kama muda wote ambao hatokuwepo ni zaidi ya muda huo, uchaguzi unatakiwa ufanywe kutafuta mtu mwingine. 

 

Kiungo wa Klabu (Ofisa uhusiano)

Kama Rais, ni jukumu lako kuwa daraja kati ya Shirika la Agora Speakers International na klabu.

Hasa, unatakiwa kuwa unajua taarifa zote mpya kuhusu masharti, matangazo, maendeleo ya mipango, mabadiliko, nk. Kwa kawaida, haya yanakuwa ni mawasiliano kupitia kundi rasmi na kutumwa kwa barua pepe kwa maofisa wote wa klabu walioandikishwa. Shirika linabadilika sana, na daima tunaongeza shughuli mpya, majukumu na kutanua mfumo wa usimamizi wa mtandaoni. Kama hautopata barua pepe kutoka kwetu kwa zaidi ya mwezi mmoja, tafadhali angalia folda ya barua taka na hakiki kuwa barua pepe ambayo umewasilisha Makao Makuu ya Agora ni sahihi.

Unatakiwa kuwa daraja kati ya klabu na bodi za usimamizi nyingine za Agora ndani ya nchi, haswa Mabalozi.

 

Mwakilishi wa Klabu

Rais wa klabu pia anafanya jukumu la uwakilishi, kuzungumza kwa niaba ya klabu kwenye matukio, mbele ya mashirika ya wahusika wa tatu, na vyombo vya habari.

Tafadhali kumbuka kuwa unawakilisha kundi, unatakiwa kutetea mawazo na nafasi za kikundi, bila kujali kama unakubaliana nayo au la. Wakati unazungumza kama mwakilishi wa klabu, unachukua jukumu tofauti kuliko pale unapojizungumzia kwa niaba yako mwenyewe.

 

Bajeti ya Klabu

Kama klabu inasimamia fedha za aina yoyote ile (bila kujali kama zinatoka kwenye ada au vyanzo vingine), wanachama wanatakiwa kuonyeshwa bajeti ya klabu mwanzoni mwa muhula na fedha zilizobaki mwishoni.

Bajeti ya klabu inaonyesha jinsi klabu itafanya matumizi na ni vyanzo gani vya fedha klabu itakuwa navyo. Rais ana jukumu la kupanga bajeti, ambayo inatakiwa kuonyesha dira yake na mkakati wa klabu, na inatakiwa kuzingatia mahitaji ya timu ya maofisa wote na maoni yao. Bajeti inatakiwa kukubaliwa na wanachama wa klabu kwa kupiga kura, kama ilivyoelezewa kwenye kipengele cha Demokrasia ya Ndani ya Klabu.

 

Majukumu Mengine

Mwisho lakini si kwa uchache, Marais wa Klabu wana majukumu yafuatayo ya ziada:

  • Kufanya uchaguzi kwa ajili ya kupata timu mpya ya maofisa wa klabu
  • Kuandaa upigaji wa kura kwa masuala yanayohusu klabu.
  • Kuidhinisha (pamoja na Mweka Hazina wa klabu) matumizi ya fedha za klabu.
  • Kusimamia data za klabu kwenye Mfumo wa Usimamiz wa Klabu wa Mtandaoni

 

 


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:49 CEST by agora.