Loading...
 

Klabu za Umma

 

Klabu za Umma ni aina ya klabu ambayo inatumika sana na ndio ambayo Shirika inahimiza kila mtu kuunda. Kuna mpango ambao unaondoa ada kwa klabu za shirika au zenye vizuizi kwa miaka kadhaa kama wataunda na kutoa ushauri kwa klabu ya umma. 

Uanachama


Klabu ya umma ipo wazi kwa kila mtu. Hamna mahitaji yoyote ya kujiunga zaidi ya uwepo wa nafasi. "Uwepo wa nafasi" ina maana mbili:

  • Kama klabu inakutana uso kwa uso kwenye ukumbi, lazima kuwe na nafasi ya kutosha kwa ajili ya wanachama wote.
  • Kama klabu inakutana mtandaoni, basi "nafasi" inahusu uwezo wa kusimamia idadi ya wanachama. Kwa mfano, japokuwa mikutano ya mtandaoni inaweza kuwa na idadi ya washiriki bila vizuizi, kusimamia wanachama 150 mtandaoni inaweza ikawa kazi sana. Kwahiyo, klabu inaweza ikaweka kizuizi cha nafasi hata kwa ajili ya mikutano ya mitandaoni hata kama sababu hazihusiana na teknolojia.
Klabu ambazo zinakutana mara kadhaa au mtandaoni tu wanaweza wakaweka vigezo kuwa wanachama watarajiwa wawe karibu kijiografia na mahali ambalo klabu imeandikishwa. Hii ni muhimu kuruhusu klabu kuhamia mikutano ya uso kwa uso muda wowote baadae bila ya kupoteza nusu ya uanachama kwasababu ya kushindwa kuhudhuria. 

Wakati hakuna mahitaji ya ujumla ya uanachama, klabu ni na zinabakia kuwa chombo binafsi ambacho ni tofauti na Agora Speakers International. Kwahiyo, uanachama ni kwa kualikwa tu na unatakiwa kukubaliwa na wanachama: kama wanachama wa klabu wanaamini kuwa mtu fulani, kwasababu ya sababu maalum, sifa bainishi, au tabia, zitazuia au kusumbua kazi za klabu, wana uhuru wa kumkataa huyo mtu kama mwanachama.

Haki ya hapo juu isitumiwe kuunda sera za kibaguzi kwa ujumla. Kama unahisi kuwa unakataliwa uanachama kwa sababu ya sera za kibaguzi kwa ujumla, tafadhali tuma malalamiko kwenda Agora Speakers International, na tutafuatilia suala hili.

Vizuizi vya Umri

Agora inaruhusu Klabu za Umma ziundwe kama "Klabu za Vijana", ambapo mahudhurio ni kwa ajili ya watu wasio na umri wa utu uzima (ambapo umri maalum unategemea na ufafanuzi wa eneo husika) na wazazi wao au walimu.

Lakini, kumbuka kuwa, hiki ni kizuizi pekee cha umri ambacho kinaruhusiwa. Kama umri wa utu uzima kwenye nchi ni miaka 18, klabu inayoweka kizuizi cha mahudhurio kuwa "Watoto wa miaka 6-18 tu na wazazi wao" ni sahihi, lakini ambazo zinaweka kizuizi cha mahudhurio kuwa but ones that limit attendance to "watoto 14-20", "watu walio chini ya umri wa miaka 30", au "wazee juu ya 60 tu", nk. hawako sahihi.

 

Mahali pa Mkutano

Klabu za umma lazima zikutane mahali ambapo wanachama wote wanaweza kufikia ili kuepuka kuunda kizuizi kisicho cha wazi kwenye uanachama. Kwa mfano, klabu ya umma haiwezi kukutana kwenye jengo ambalo, kwasababu ya ulinzi, linafikiwa tu na wafanyakazi wa kampuni kwasababu hiyo inazuia wengine ambao sio wafanyakazi kuwa wanachama. Hii pia inatumika kama mahitaji au juhudi ambazo baadhi ya wanachama watakiwa kufanya ili kufikia ukumbi ni juu zaidi kuliko wanachama wengine. Kwenye mfano wa hapo juu, kama wasio wafanyakazi wanaweza kuingia tu kwenye jengo baada ya uchunguzi na vituo vingi vya ukaguzi ambavyo vinahitaji kupekuliwa, kuacha vitu vyao vya binafsi nje, nk, basi mahali hapo pa mkutano hapatafaa kwa Klabu ya Umma licha ya uwezekano wa kila mtu kuhudhuria.

 

Klabu za Umma ndani ya makampuni

Klabu ambazo zinakutana kwenye eneo la kampuni ya biashara lakini inaruhusu kila mtu kuwa mwanachama (ikiwemo wasio wafanyakazi) na haizui maudhui wa hotuba bado inazingatiwa kuwa Klabu ya Wazi ya Umma.

 

Wageni na Wanaozuru

Klabu za Umma lazima wakubali wageni na wanaozuru kutoka klabu nyingine. Kama wasio-wanachama wengi wanania ya kuhudhuria na kama kuna nafasi ya kutosha (au siti za sibayana kama mkutano ni kwenye jukwaa la mtandaoni) kwa ajili yao wote, orodha inayofuata ya kipaumbele inatumika:

  • Maofisa wa Shirika la Agora Speakers International na wanachama wa Bodi ya Wakurugenzi wa Agora Speakers International (kwa ajili ya ukaguzi, uadilifu, na ukurufunzi)
  • Mabalozi wa Agora
  • Wanachama wa Agora kutoka klabu zingine
  • Wageni wasio wa Agora    
Haki ya makundi ya hapo juu kutembelea Klabu za Umma haimaanishi kuwa wanaruhusiwa kufanya majukumu yoyote wanayotaka. Ni chaguo la klabu kuwapa majukumu ya kufanya wakati wa mkutano wa klabu.

Mapendekezo yetu ya majukumu yaliyo ruhusiwa ni kama ifuatavyo:

  • Mabalozi wa Agora: Watathmini, majukumu ya uongozi wa vipengele (kwa mfano, Msimamizi wa mdahalo, Kiongozi wa Hotuba za Papohapo), na warsha
  • Wanacham wa Agora kutoka klabu zingine: majukumuu yote
  • Wageni wasio wa Agora: Majukumuu yote isipokuwa Utathmini wa Hotuba na Hotuba zilizondaliwa
Haki ya kutembelea Klabu ya Umma haitakiwi kutumiwa sana mpaka kufikia wakati ambapo wanaotembelea anakuwa kama mwanachama wa klabu bila ya majukumuu ya kikamilifu ya uanachama wa klabu. Isipokuwa kwa kundi la kwanza (maofisa na Wanachama wa Bodi), klabu ina uhuru wa kukataa mahudhurio ya wasio wanachama kama wakianza kutumia haki hiyo kama wanachama bandia ndani ya klabu. Ingawa ni vigumu kutoa mwongozo maalum, kanuni nzuri ni kuwa kila mtu anayetembelea klabu zaidi ya mikutano mmoja kati ya minne anatakiwa kualikwa kuwa mwanachama.

Isipokuwa kama kuna gharama kwa kila mtu na kwa kila mkutano ambazo zinatakiwa zilipwe (kwa mfano, kama chakula cha jioni kinahudumiwa kwa kila anayehudhuria), makundi yote ya hapo juu yanatakiwa kuhudhuria mkutano bure. Kumbuka kuwa wanaotembelea wanaweza tu wakatozwa kama wana athari ya moja kwa moja na ya kupimwa kwenye gharama za jumla za mkutano. Kwa mfano, kama klabu inakodi mahali pa mkutano kwa mwezi au kwa kila mkutano, gharama ya kukodi haitobadilika kwasababu ya anayetembelea, na kwahiyo kwenye suala hili, wageni hawawezi kutozwa.

 

Vigezo vya Kifedha

Klabu za umma zinaweza zikachagua kukusanya ada kutoka kwa wanachama wake kwa ajili ya uendeshaji. Kwenye suala hili, wanatakiwa kufuata vipengele vya masharti ya fedha za klabu.

Klabu za umma hazilipi ada yoyote kwa Agora Speakers International - hamna ada yoyote ya kuanzisha (kuunda), ya kipindi fulani au ya kila mwanachama.

Mwisho, klabu za umma zinatakiwa kutumia mfumo wa mtandaoni wa uhasibu wa Agora kwa ajili ya kufuatilia fedha zao na kwa ajili ya kuripoti.

 

Taarifa za Kuorodhesha

Taarifa kuhusu klabu za umma ni.... za wazi. Zifuatazo ni taarifa ambazo zinasambazwa kwa kila mmoja na lazima maofisa wa klabu wahakikishe ni za hivi karibuni:

tAARIFA ZA KLABU ZA KUSAMBAZWA
Aina ya Taarifa Zinasambazwa kwa
Jina la klabu, namba, na siku ya kuanzishwa Hadhira
Ratiba ya mkutano Hadhira
Mahali pa mkutano Hadhira
Maofisa wa klabu na taarifa zao za mawasiliano Wanachama wa Agora
Muundo wa ada Hadhira
Fedha za klabu Wanachama wa Agora
Vizuizi vya Kutembelewa  Hadhira
Vizuizi vya Maudhui ya Hotuba Hadhira
Taarifa za mawasiliano za klabu Hadhira
Tuzo na Medali Hadhira
Lugha za Klabu Hadhira

 

Uangalizi wa Muundo wa Kielimu wa Agora

Klabu zinatakiwa kufuata na kuzingatia Muundo wa Kielimu wa Agora na Mpango wa Kielimu wa Agora. 

Hii, maalum, inamaanisha kuwa kila mkutano unatakiwa kuwa na angalau: 

Mahitaji yafuatayo lazima pia yazingatiwe:

  • Hotuba zote, majukumu, na vipengele vya mikutano lazima vithathminiwe kulingana na vigezo vilivyowekwa kabla.
  • Vipengele vyote vya mkutano lazima uzingatie muda. Hamna mshiriki yoyote hataruhusiwa kuzungumza bila kizuizi cha muda.
  • Hotuba nyingi ambazo zimeandaliwa lazima ziwe kutoka Njia ya Kielimu ya Agora.
  • Shughuli nyingi lazima ziwe kutoka Shughuli za Mikutano ya Agora.
  • Majukumu mengi lazima yawe kutoka Majukumuu ya Mikutano ya Agora.
Ni sawa kabisa kama wanachama watatoa hotuba maalum au hotuba kutoka mipango mingine ya kielimu ambayo wanayo, maadam inajulikana kabla na inatathminiwa. Ni sawa kabisa kama klabu ina shughuli tofauti na zile ambazo zimeorodheshwa kwenye mpango wetu. Sharti la "wingi" ina lengo la kuhakikisha kuwa klabu hazifanyi vitu tofauti kutoka kila klabu za Agora zinafanya kwa kawaida, kwasababu itakuwa haina maana ya kuwa ndani ya Agora.

Kizuizi maalum kwenye klabu za umma ni kuwa haziwezi kutumiwa kutangaza au kukuza bidhaa, huduma, au shirika la wahusika wa tatu, usiweke vizuizi vya maudhui ya hotuba kwa lengo hilo.

 


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:43 CEST by agora.