Loading...
 

Leo Tunasafiri Kwenda

 

Demonization

 

 
Activity Summary
  • Tafuta kundi la watu ambalo linachukiwa kwenye mazingira yako. 
  • Tafiti kundi hilo na tafuta kitu kimoja kuhusu wao ambacho unakipenda kiukweli - utamaduni, muziki, fasihi, dansi, chakula, mila, mavazi, desturi, nk...
  • Wasilisha hotuba ya kutaarifu kwenye hiko kitu kimoja ambacho unakipenda bila kutetea kikundi au kuwaomba watu kuwaonea huruma.
  • Usielezee lengo la kipengele hiki.
 

Utambulisho wetu wa kikundi

Wanadamu ni viumbe wa makundi. Kutoka kwenye mtazamo wa mageuzi, wanadamu wanahitaji msaada wa muundo wa jamii ili kuweza kuishi. Watoto wa binadamu wana utegemezi wa muda mrefu sana kwa wazazi wao kuliko spishi zote, na hata baada ya hapo, Homo Sapiens Sapiens hana ujuzi maalum wa kukimbia, kupanda miti, au kuogelea. Hatuna viungo vya kuhisi ambavyo vimeendelea kimaalum. Tunavutwa kutafuta ndugu wa karibu na kuunda vikundi ambavyo kwa ujumla vina uwezo mkubwa wa kuongeza nafasi ya kuishi - kutoka kuwinda pamoja mawindo makubwa mpaka kugawanya kiufasaha kazi mpaka kutafuta wenza wanao wanaofaa.

 


Pale utakapoingia kwenye mtego wa chuki, unaweza kurubuniwa kirahisi kama mafahali kwenye michezo ya ng'ombe ya Uhispania. (Picha: Francis Heylighen )
Pale utakapoingia kwenye mtego wa chuki, unaweza kurubuniwa kirahisi kama mafahali kwenye michezo ya ng'ombe ya Uhispania. (Picha: Francis Heylighen )

Kwenye zama za sasa, hamna kitu kilichobadilika. Bado tuna na matakwa makubwa ya "kustahili kuwa mmoja wao" kwenye kundi fulani. Lakini, kama ikichukuliwa kupita kiasi, hitaji hili linabadilika na kuwa kitu wanaanthropojia wanaitwa "ukabila wenye sumu" - uzingatiaji bila masharti wa kikundi chako mpaka unakuwa hauna ufahamu, unalazimisha kauli, na ukatili dhidi ya makundi mengine.

Kama kitu kikiwa cha bila ufahamu au kimekuwa cha kawaida, hauna tena uthibiti nacho. Hauchunguzi kwa kina kama kile unachosoma au unachoambiwa kina maana, maadam kinaendana na utambulisho wa kikundi. Kibaya zaidi - mwitikio wako unakuwa unatabirika. Hivyo, unakuwa mlengwa rahisi wa upotoshaji - kama vile ng'ombe dume (fahali) anavyoweza kufanywa akimbie kwenda mwelekeo wowote ule kwa kupeperusha mbele yake kitu chochote ambacho anadhani ni cha hatari.

 

Chuki (Udhalilishaji)

Chuki ni mbinu inayotumika sana kuchochea moto wa ukabila wenye sumu na kuwafanya watu wengi kuwa na tabia maalum. Inajumuisha kuhusisha tabia hasi na watu wa kundi tofauti. Makundi hayo tofauti yanaweza kuwa ya kijiografia (kuwa na chuki dhidi ya watu wa nchi au mikoa mingine) ya kikabila (chuki dhidi ya watu wa rangi fulani maalum), kidini (chuki dhidi ya waumini wa dini fulani), nk. Unaweza kuona mifano mingi ya kuwaona waovu kwenye picha ya kwanza ya kazi hii.  

Mara nyingine chuki inaanza na mlengwa rahisi - kama vile kiongozi au mwakilishi anayejulikana wa kundi fulani lililochaguliwa. Kwa maneno ya Taasisi ya Cato:

"M ara utakapoanza kumchukia rahisi au kiongozi wa nchi,  unaanza kupandikiza chuki  ya kudumu inayochochewa na itikadi kwenye mioyo na akili za Wamarekani na inahalalisha matendo yoyote ya uhasama dhidi ya nchi na watu wake kwenye siku za baadae."

 

Licha ya kuwa waziwazi, kwa kawaida ina ufanisi kwasababu ya picha dhahiri ambayo inatengeneza kwa hadhira na kwasababu inatengeneza hisia ya uoga dhidi ya makundi ambayo mtu anayependa. Mara uoga au chuki ya kutosha itakapopandikizwa, anaweza akaamrishwa kufanya vitu ambavyo kwa kawaida asingeweza kufanya maishani, mpaka kufikia hatua ya kuua wengine au kujitoa mhanga.

Hermann Göring, mmoja ya viongozi mashuhuri wa chama cha Nazi, mwanzilishi wa Gestapo, na Kiongozi wa Jeshi la anga cha Ujerumani (Luftwaffe), alionyesha hili vizuri sana na tamko lifuatalo wakati wa Kesi za Nuremberg za Uhalifu wa Vita:

Ndio watu hawataki vita. Kwanini mtu masikini shambani atake kuhatarisha maisha yake kwenye vita wakati kitu kizuri zaidi anachoweza kupata kutoka vita ni kurudi shambani kwake mwili wake ukiwa ni mzima? Kiuhalisia, wananchi wa kawaida hawataki vita; sio wa Urusi sio wa Uingereza sio wa Marekani, na sio pia wa Ujerumani. Hilo linaeleweka. Hata hivyo, ni viongozi wa nchi ambao wanaamua sera za nchi, na ni jambo la rahisi sana kuwavuta watu wafuate, ikiwa kama ni demokrasia au udikteta wa kifashisti au bunge au udikteta wa kikomunisti.
Daima watu wanaweza kuletwa kufanya matakwa ya viongozi. Ni rahisi. Unachotakiwa kufanya tu ni kuwaambia kuwa wanavamiwa na kuwashutumu wapinga vita kuwa hawana uzalendo na wanaweka nchi kwenye hatari. Inafanya kazi sawa kwenye nchi yoyote ile. 
 

 

Japokuwa kuchukia makundi mengine na viongozi wake vimekuwepo tangu mwanzo wa historia, imesambaa sana kwenye zama hizi za kisasa, ikisaidiwa na usambaaji wa mitando ya kijamii. Amnesty International mwaka 2016-2017 walitoa ripoti kutoa tahadhari dhidi ya hatari ya aina ya mbinu hizi.

Kwanini uwe na chuki?

Watu ambao wanakuwa na chuki kwa vikundi fulani wanafanya hivyo kwa sababu kuu mbili:

  • Kulazimisha ajenda yao wenyewe. Kwa mfano, ni rahisi zaidi kuongeza matumizi ya jeshi kama watu wanadhani maisha yao yapo hatarini. Ni rahisi zaidi kuongeza bajeti za idara za polisi kama watu wanaamini kuwa kuna ongezeko kubwa la wahalifu. Kiukweli, kuonyesha uovu ni njia rahisi na nafuu ya kulazimisha ajenda.
     
  • Kuhamisha kitovu cha umakini kwenda sehemu nyingine au kusahaulisha. Kwa mfano, kama chama chako kikikutwa kimeiba pesa za umma, ni rahisi sana kupitia kipindi kile kama vyama vyote vikinyooshea kidole masuala mengine.

 

Kupambana na ukabila wenye sumu na udhalilishaji

Kupambana na ukabila wenye sumu, udhalilishaji, na ubaguzi, kwa ujumla, sio suala la kirahisi, haswa kama yaliyotajwa wanafanywa kwa chini chini na kwa njia isiyoonekana kirahisi.

Kama video hii fupi ya mzaha inavyoonyesha, kinachoitwa ubaguzi dhahiri  kinaweza kikajitokeza kama athari ya kitu kilichochochezwa na jamiii, hata kama watu wanaohusishwa wanajua uwepo wake na jinsi isivyofaa au kupendwa. 

Mmoja anaweza kufikiri kuwa ukabila unaweza ukapingwa kwa kuelezea kiuwazi kuhusu ubaya wa chuki au ubaguzi na kuwaambia watu wasitende uovu huo. Japokuwa hiyo ina baadhi ya matokeo, tafiti inaonyesha kuwa matokeo haya ni ya muda mfupi. Hii ni moja ya sababu kwenye mradi huu, hotuba yako haitakiwi kuwa ya kuwaomba watu kuacha hiki au kile, au kujaribu kutoka hoja zenye busara kuhusu hilo. 

Kuna njia nyingi ambazo tafiti zimeonyesha kufanya kazi dhidi ya chuki na ubaguzi kwa ujumla. 

Utoaji wa mifano ya kupinga iliyo chanya

Hatua ya kwanza ni kuwaweka wazi watu kutoka makundi yanayobaguliwa ambao wana sifa tofauti na zile ambazo ubaguzi unaonyesha ("kupinga ubaguzi "). Kukiwepo uwazi wa kutosha,  ubaguzi huu utapungua kwa kiwango kikubwa sana. Kwa mfano, kama ubaguzi ni kwamba "majipsi ni wezi", ubaguzi wa kupinga utakuwa kuzungumzia Waroma wanaoheshimiwa au Waroma ambao wamefanikiwa au wenye tabia bora. 

Habari nzuri kuhusu upingaji wa ubaguzi ni kuwa zina ufanisi hata kama zimefikiriwa tu. Hii ni mbinu inayotumiwa kiupana kwenye taswira - ambapo kufikiria au kudhania tu suala linakusaidia kukuandaa. Kwa njia sawa, kufikiria tu kuwa Waroma ni watu wa heshima inasaidia tayari kupunguza ubaguzi.

Tahadhari -  tafiti inaonyesha kuwa mifano mikali ya kupinga inakuwa na athari ya bumerangi, inaimarisha ubaguzi. Utaratibu sawa na "ah, lakini hiyo itakuwa ni kasoro ambayo haithibitishi sharti " inasisimuka kwenye ubongo wetu. Kwahiyo kama ubaguzi ni kuwa "wanawake ni wadhaifu", kwa mfano, mifano ya kupinga inatakiwa kuwa wanawake jasiri wa kawaida, na sio kama Malkia Elizabeth au Joan wa Arc (Jeanne d'Arc).

 

Kuna tokeo moja chanya la kuwasilisha mifano ya kinyume ya ubaguzi. Tafiti zinaonyesha kuwa watu wakilazimishwa kukabiliana na mifano ya kupinga ya imani na mifumo yao, wanakuwa nyumbufu zaidi na wafikiriaji wabunifu. 

 

Kuvunja mzunguko huu

Presha na desturi za kijamii (aidha za kweli au zinazodhaniwa) zina nafasi kubwa sana kwenye utengenezaji na uendelezaji wa baguzi hizi. Imani zetu zinaimarishwa kama tunafikiri waliowengi kwenye jamii wanafikiria hivyo hivyo pia. Kiukweli, majaribio ya ukubalifu ya Asch yanaonyesha kuwa presha za kijamii zinaweza kutufanya tukakataa kufuata maarifa na kubadilika kwenda mawazo ambayo ni wazi na dhahiri sio sahihi.

Tafiti zinaonyesha kuwa watu wakigundua kuwa wenzao hawana chuki kama za kwao, ubaguzi unapungua. Kiukweli, moja ya malengo ya mradi huu ni kutoa ushuhuda mathubuti ambao unasema, "Habari, nipo hapa, na ninafikiri tofauti na watu hawa. Kama unaamini chuki inachokuambia, nipo hapa kusema kuwa sina maoni sawa kama wewe". 

 

Kuchunguza kwa umakini ujumbe kutoka nje, na imani zetu wenyewe

Tunaweza kuchukua hatua kubwa dhidi ya sumu ya ukabila kwa kuchunguza, kuthibitisha ukweli, na kutoamini kirahisi taarifa zozote ambazo tunapokea, haswa kama zina maneno ya kuhukumu au kujumuisha. Hii ni sehemu ambayo tutaifanyia kazi sana kwenye njia ya Umakinifu.

Huu hapa ni mfano mfupi ya jinsi chuki inaweza ikasambazwa taratibu na kwa chinichini. Kwasababu ya janga la COVID, nchi nyingi duniani zilibidi zifunge mipaka yake ili kuthibiti uwezekano wa kirusi kusambaa zaidi. Je unaweza kuona tofauti ndogo kwenye simulizi na jinsi kufunga mipaka inavyoonyeshwa kwenye vipande hivi viwili vya gazeti la NY Times?

Double Standards

 

Kujishughulisha na harakati za ushirikiano na wawakilishi wa makundi.

Hakika, kufanya kazi au kuwa pamoja kidogo kwenye maana isiyo ya kukabiliana au kubishana na wawakilishi wa makundi haya yanayochukiwa  inapunguza ubaguzi kwa kiasi kikubwa muda unavyoenda. Uwezo wa kuthibiti kuhukumu, inafanya kazi tofauti na aina ya watu, kuwa nyumbufu, mbunifu, na kuwa muwazi wa fikra ni vigezo vya muhimu kwa viongozi wa siku hizi, na tunafanya kazi kuendeleza tabia hizi kwenye mradi wa Uongozi wa Agora.

 

Kazi Kuu

Kwenye mkutano wa kipengele cha "Leo Tunasafiri Kwenda..."  utahitaji kufanya vitu hivi viwili:

Utafiti

1 Kuwa makini na mwangalifu kugundua ishara za chuki zinazokuzunguka - aidha kwenye mitandao ya kijamii, kwenye maoni ya marafiki, runinga, magazeti nk, na kujua kundi ambalo linachukiwa. Labda hata wewe mwenyewe unafanya tabia ya aina hiyo?. Ni muhimu kwa kazi hii kuwa chuki lazima iwe inatokea kwenye muktadha wako , sio sehemu nyingine au kimaandishi. Kama unaishi Uswidi, usizungumzie kuhusu Waafrica ambao wanachukiwa Uhispania. Labda una makundi ya karibu zaidi.

Kwenye nchi nyingi, hautohitaji kutumia nguvu sana kufanya hivyo. Urusi na Marekani wanachukiana sana kwenye himaya zao za nguvu. Hilo pia linaweza likasemwa kuhusu wahusika wa Mashariki ya Kati. China na Japani ni "tamaduni" nyingine. Kiukweli, ni rahisi kutafuta kwenye mtandao kiutani (lakini pia kiukweli) ramani ya "nani anachukia nini," kama mfano wa ramani hii ya "chuki barani Ulaya": 

Hatemap Europe

Chuki nyingi sio kwa wazi basi kwa chini chini. Zoezi zuri la kugundua hili ni kwa kusoma/kuangalia watoa maoni wanaojulikana (inaweza kuwa vyombo vya habari vya jadi, blogu zinzojulikana, waraghibishi, nk) na kuchunguza vipande ambavyo vinakufanya kutompenda, kumhukumu au kumlaani mtu. Kitu chochote kinachokufanya kupata hisia hasi kwa kundi la watu.

Hotuba ya Klabu

 

2 Pale utakapotambua kundi ambalo linachukiwa au kubaguliwa, lengo ni kutafiti kundi hilo na kuwasilisha hotuba ya dakika 3-5 inayoonyesha kitu changu kuhusu kundi hilo ambalo limevuta umakini wako. 

Utakuwa unatumia mbinu mbili kwenye hotuba hii: 

  • Kuwasilisha mfano mmoja au mifano miwili chanya ya kinyume.
  • Kutuma ishara dhahiri kuhusu imani za wanaobaguliwa ambazo hazijaenezwa. Baada ya yote, kuzungumzia kwa uzuri kundi ambalo linalobaguliwa, utakuwa ni mfano hai kuwa kuna watu wenye imani tofauti.

Hotuba inatakiwa kuzingatia kikamilifu vitu chanya ambavyo umevigundua. Hivi vinaweza kuwa chochote ambacho unaweza kupata: kutoka hadithi mpaka chakula, kutoka mila mpaka ujenzi, kutoka tamaduni mpaka sanaa, kutoka matukio ya kihistoria mpaka maendeleo ya sayansi ya kundi hilo. Hotuba inatakiwa kuhabarisha na kuwa ya ukweli, sio ya kushawishi. Haujaribu kushawishi mtu yoyote kuhusu kitu chochote - wewe unaweka kitu chanya kuhusu kundi linalobaguliwa. 

Ni muhimu sana ukipende kile unachozungumzia. Usizungumzie vitu ambavyo "ni vizuri kinadharia" au "kila mtu anatakiwa kukipenda" - zungumzia vitu ambavyo wewe binafsi unafanya.

Ni muhimu pia kufanya hotuba kuhusu kitu chenye umuhimu  kwa kundi (kwa maneno mengine, kuhusu vitu ambavyo vipo jinsi vilivyo kwasababu ya maamuzi  au matendo hai ya kundi hilo maalum).
Kwa mfano, fikiria unataka kuzungumzia kuhusu Wabulgaria. Haina maana kutoa hotuba kuhusu uzuri wa milima na maziwa ya Bulgaria yalivyo kwasababu - kama nchi nyingine yoyote duniani - ni historia tu bahati tu kuwa Wabulgaria wanaishi kijiografia mahali wanapoishi, na milima na maziwa yangekuwa mazuri tu kama Wachina, Wajapani, Majipsi au kundi lingine la watu wangekuwa wanaishi katika sehemu hiyo (Kiukweli, uhalisia ni tofauti kidogo - sifa hizi za kijiografia zinaumba utamaduni baada ya muda, mila, na hata jinsi kundi linavyoona dunia. Hata hivyo, kwa lengo la mradi, na kwasababu uumbaji huu unatokea katika kipindi kirefu sana, tunadhania haina umuhimu).
Hata hivyo, unachotakiwa kufanya, ni kuzungumzia mahusiano kati ya kundi na mazingira yake kwasababu hayo ni maamuzi yao kabisa. Kama kundi fulani linaweka mazingira safi, inathamini rasilimali, ina sera za kujitosheleza za maendeleo, nk. Hayo yote ndio yanahifadhi uzuri wa milima na maziwa ambayo yapo -  hiyo ni mada ambayo inafaa kwa ajili ya hotuba.

 

Kama hotuba zote, jaribu kuwa makini na mada. Hauna lisaa limoja la kuzungumza, jaribu kutaja pointi moja au mbili za muhimu na uzielezee. Kwa mfano, badala ya kuwasilisha historia yote na hadithi za majipsi kwa dakika 5, kuwa makini na aidha tamasha moja maalum au tamaduni moja maalum, na ielezee kwa undani.

Hotuba haitakiwi: 

  • Kutaja kundi ambalo linafanyiwa uovu.
  • Kujadili kwanini umechagua kundi moja badala ya jingine.
  • Kuonea huruma, huzuni kundi hilo, au kufikiria sana suala au magumu yao. Kwa mfano, kama umeamua kuchagua kundi la wahamiaji au wakimbizi, mada ya hotuba yako haitakiwi kuwa jinsi ilivyokuwa vigumu wao kufika kwenye nchi yako au jinsi vita ilivyokuwa mbaya nchini kwao.
  • Kuwahimiza hadhira kuwapenda au kufanya chochote kile. Kumbuka - hii sio hotuba ya kushawishi ambayo inaishia na wito wa kutenda (Kumbuka utafiti ulichoonyesha - utafanikiwa tu kudhani kuwa umebadilisha mawazo ya watu , lakini kiukweli, ubaguzi wao wa zamani utarudi muda tu watakapotoka kwenye ukumbi)

Kama utafanya chochote kilichotajwa hapo juu, utakuwa tu unatengeneza upinzani ambao unashinda lengo la shughuli. 

Usizidishe kupita kiasi. Kumbuka utafiti wa mifano ya kinyume sana ya hapo juu. Ukijaribu kwenda kwenye hali chanya kupita kiasi, ukijaribu kuonesha kundi ulilochagua kama zuri zaidi duniani, au muziki/chakula chao nk ni vya kipekee na kujaza hotuba yako na sifa sana, upo katika hatari ya kusababisha athari ya bumerengi (hoja au pendekezo ambalo humrudia mtoaji na kumdhuru)

Kichwa cha habari cha hotuba kinatakiwa kuwa "Leo  tunasafiri kwenda... ". Kwa mfano:

  • Leo tunasafiri kwenda Urusi
  • Leo tunasafiri kwenda California 
  • Leo tunasafiri kwenda ulimwengu wa majipsi.
  • nk.

Utathmini 

Mradi unatathminiwa kulingana na kadi ya utathmini iliyowekwa hapa. 

Kumbusho kwa mtathmini: Kuna mstari mwembamba kati ya kuongea kuhusu kundi na wapi na jinsi wanavyoishi na kutoa hotuba ya aina ya "filamu" ambayo mzungumzaji anaelezea tu kirahisi kuhusu sehemu nzuri aliyokwenda. Mchanganyiko wa kawaida kwenye huu mradi - kutoka kwa wazungumzaji ambao hawasomi maelezo kwa ujumla - ni kufikiri kuwa "Leo tunasafiri kwenda..." ni kama kichwa cha habari kinavyosema - kwenda sehemu fulani nzuri na kuelezea hadithi kuhusu hiyo sehemu.  Dhahiri, hilo sio suala, na kama ukiona hotuba inayowasilishwa ni ya aina hii, unatakiwa ueleweshe kwa uwazi kuwa malengo hayakutimia, elezea kwanini, na pendekeza kuwa mzungumzaji arudie jukumu hili kwenye mkutano wa siku za mbeleni. 

Kwa upande mwingine, kwasababu mzungumzaji kwa maksudi hatosema kwa uwazi kundi ambalo analizungumzia, mara nyingine inakuwa vigumu kugundua kama tupo kwenye suala la kwanza. Hii ni ukweli hususan kwenye mikutano ambayo watu wanaoshiriki ni kutoka tamaduni na nchi tofauti: kundi fulani linaweza likawa linabaguliwa kwenye mazingira ya mzungumzaji lakini sio ya kwako. 

Kwahiyo utakapoamua kutathmini hotuba ya "Leo tunasafiri kwenda (kiuhalisia, siku chache kabla ya mkutano), ni wazo zuri kumtafuta mzungumzaji na kumuuliza kuhusu kundi ambalo amelichagua. Hii pia itakuwa ni kama ukumbusho mdogo wa kuwa hotuba sio wa aina ya kitalii.
 

 

 

Rasilimali

 


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Thursday May 27, 2021 15:46:56 CEST by zahra.ak.