Loading...
 

Njia ya Msingi ya Kielimu

 

Njia ya msingi ya kielimu ina miradi 16 iliyopangwa kwenye makundi matatu ambayo yanakufundisha ujuzi muhimu wa msingi wa uzungumzaji wa mbele ya hadhira.

Kila mradi una kikomo maalum cha muda, malengo, vizuizi vya vitu ambavyo vinaweza kutumiwa (visaidizi vya kuona, mimbari, nk.…), na mada za hotuba. Miradi inatakiwa kufanywa kikamilifu kwa mpangilio. 

Kwa ujumla, unaweza kuzungumzia chochote ukipendacho, isipokuwa uzungumzaji wa mbele ya hadhira. Hii inamaanisha kuwa, kwa mfano, mradi namba 11 ("Utofauti wa Sauti"), hauwezi kufanya hotuba kuhusu utofauti wa sauti. Lengo la kizuizi hiki ni kukusaidia kutambua kuwa mbinu zote (lugha ya mwili, utofauti wa sauti, ucheshi, nk....) ni zana za kusaidia ujumbe mkuu, lakini havitakiwi kuwa ujumbe mkuu wenyewe. Angalia makala ya "Maudhui ya Hotuba" ili kupata maelezo ya kina zaidi ya aina gani ya maudhui ni sahihi kwa ajili ya hotuba. 

Kila mradi una kadi ya alama ya utathmini maalum ambayo inatakiwa kujazwa na mtathmini wa hotuba. Kadi hizi za alama zipo chini ya kurasa ya kila mradi.

 

Eval Form 1

 

Eval Form 2

 


Pale utakapokuwa umemaliza Njia ya Msingi ya Kielimu, utapata cheti na beji inayoendana.


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:58 CEST by agora.