Loading...
 

Dhumuni la Klabu

 

 

Koka Prasad, akiongoza klabu ya Vikasha Orators
Koka Prasad, akiongoza klabu ya Vikasha Orators

Klabu za Agora Speakers zinatoa mazingira ya kusaidia na ya kirafiki ambapo wanachama wanajifunza na kufanya mazoezi ya ujuzi wa msingi wa kuzungumza mbele ya hadhira na uongozi. Hapo utakuta sio tu mazingira mazuri yanayohimiza kufanya mazoezi, lakini pia utakuwa sehemu ya jamii ambayo itakusaidia kwenye miradi yako, utafahamu wengine waliyopitia, na utapata maoni yenye thamani ya jinsi ya kujiboresha. Unaweza pia ukapata mkufunzi ambaye atakuongoza kwa jinsi unavyoendelea kwenye miradi ya kwanza ya njia ya msingi.

Ndani ya klabu ya Agora Speakers, hamna "wataalam" au "walimu" (na mikutano ya klabu sio - kwa ujumla - "semina" au "warsha") - kila mmoja yupo hapo kwa ajili ya mlolongo wa maendeleo yake mwenyewe wa kujifunza, kila mtu ana kitu cha kujifunza na cha kuboresha, kila mmoja ni rika lako na mna haki sawa.

Unaweza kufikiria klabu kama "visanduku vya mchanga" ambapo unajifunza kuthibiti wasiwasi wako, uwoga wako wa jukwaa, au sehemu ya kushinda aibu yako. Watu wengi pia wanatumia klabu kufanyia mazoezi hotuba zao maalum ambazo wanawasilisha sehemu nyingine - kutoka hotuba za msimamizi wa bwana harusi, mpaka uwasilishaji wa kawaida wa mikutano na hotuba kuu kwenye mikutano mikubwa.

 

Klabu kisheria ni mashirika ambayo yanajitegemea yenyewe, yamejitenga na Agora Speakers International lakini wana uhusiano nao. Kwahiyo, tunajaribu kuweka usawa kati ya kuhakikisha wanachama duniani kote wanapitia vitu sawa bila kujali ni klabu gani wanahudhuria na kwa wakati huo huo tunawapa klabu uhuru na tunawaacha wajiendeshe wenyewe, wawe wabunifu na wavumbuzi kwa ajili ya manufaa ya shirika zima.

Mikutano ya Klabu

Klabu zinaweza kukutana kwa Kiingereza au kwa lugha nyingine nyingi, na baadhi ya klabu zinatumia lugha mbili. Japokuwa Kiingereza ndio lugha "rasmi" ya kufanyia kazi ya Agora Speakers, tunahimiza sana klabu na makundi watumie lugha zao za nyumbani kufikia watu wengi iwezekanavyo. Kwa ukweli, unaweza kukuta baadhi ya watu wanakuja kwenye klabu ili kuendeleza uthibiti wao wa lugha hiyo.

Klabu inaweza kukutana uso kwa uso, au kwa mtandaoni, au mchanganyiko wa vyote viwili. Faida kubwa za kielimu zinapatikana kwenye mikutano ya uso kwa uso, na kiuhalisia, Mpango wetu wa Kielimu unahitaji kuhudhuria japo baadhi ya mikutano ya uso kwa uso ili uweze kuimaliza.

Mkutano wa klabu sio zoezi la kijamii la papohapo ambapo wanachama wanakutana tu na kuzungumza lakini ni tukio ambalo limeandaliwa kiuangalifu likiwa na Ajenda maalum na unaongozwa na Kiongozi wa Mkutano (ambalo ni jukumu la kujitolea ambalo linakuwa na mtu tofauti kwenye kila mkutano). Kwenye mkutano, utaona "vipengele" au "shughuli/zoezi" tofauti, kama vile "Leo tunasafiri kwenda", "Hotuba za Papohapo", "Hotuba Zilizoandaliwa", nk.:

 

Meeting Sections

 

Kuna takriban shughuli au mazoezi dazeni ambayo yanaweza kutokea kwenye mkutano wa klabu, na yanaendelea kukua. Tuna sura maalum yenye orodha kamili. Kila shughuli au zoezi linafunza seti tofauti za ujuzi. Huu hapa ni muhtasari wa baadhi ya shughuli ambazo zipo kwa sasa:

 

Activities

 

 

Nani anafanya shughuli au zoezi gani? Hili linaamuliwa na wanachama wenyewe, ambao wanajitolea kufanya majukumu kwenye mikutano, kulingana na vitu vinavyowavutia na ujuzi ambao wanataka kujifunza au kuufanyia kazi.

Klabu pia zinaanda shughuli nyingine nyingi, kama vile sherehe, mashindano, matukio ya uongozi, sherehe, na mengine mengi.

 

Muda na Utathmini

Kwa kawaida, mikutano inachukua kati ya lisaa limoja na masaa mawili, japokuwa tumeona hata mikutano ya masaa manne kwenye baadhi ya klabu.

Shughuli zote zina kikomo cha muda ambao umewekwa - mtu hawezi tu kuchukua jukwaa na kuwasilisha hotuba ya masaa manne. Kuna kiwango cha chini na cha juu cha muda wa kila shughuli/zoezi, na yameelezewa kwenye Ajenda:

 

 

Agenda Timing

 

 

Ili kujifunza na kujiboresha, kila mshiriki anapokea maoni kuhusu utendaji wake kutokana na vigezo vya utathmini wa shughuli au zoezi hilo. Kwa kuongezea, wanachama na wageni wanaweza kutoa maoni yao wenyewe ya kawaida.

 

Evaluation

 

Aina ya Shughuli/Zoezi

Kama ilivyoelezewa awali, aina nyingi za shughuli au mazoezi yanafanywa kwenye mikutano ya klabu.

Shughuli nyingi (kama vile Hotuba za Papohapo, Wazo la Siku, nk.) daima yana muundo sawa na malengo ya kielimu. Japokuwa yanabadilika maudhui (ni wazi, sio kila mtu atazungumzia kuhusu kitu kimoja kwenye kipengele cha Wazo la Siku), dhumuni halibadiliki.

Sio hivyo na shughuli ya Hotuba Zilizoandaliwa. Kila Hotuba Iliyoandaliwa ni mradi ambao ni sehemu ya mfululizo ambao unaunda Njia ya Kielimu. Kila mradi una malengo mathubuti ambayo yanatofautiana kutoka mradi mmoja mpaka mwigine. Kwa mfano, mradi mmoja unaweza kuwa kuhusu utofauti wa sauti, mwingine kuhusu visaidizi vya kuona, na mwingine kuhusu kutumia hisia. Angalia Muhtasari wa Mpango wa Kielimu kwa maelezo ya kina zaidi.

 

 


Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:15 CEST by agora.