Loading...
 

Dibaji

 

Karibu kwenye toleo la tatu la Mwongozo wa Agora - kitabu ambacho kinaelezea kila kitu kuhusu Shirika la Speakers International: sisi ni wakina nani, tunafanya nini, jinsi gani unaweza kushiriki kwenye klabu zetu, na hata jinsi ya kuanzisha na kuendesha klabu. Kitabu hiki bado kinazingatia kipengele cha uendeshaji wa klabu. Njia za Kielimu zenyewe zitakuwa ni kiini cha vitabu tofauti.

Mengi yamebadilika tangu toleo la mwisho, takriban miaka mitatu iliyopita. Tumejifunza kutoka yale tuliyopitia (na kutoka makosa yetu!), na tumepanua zaidi kila sehemu ya nyaraka na maelezo zaidi, vidokezo zaidi, ushauri zaidi wakati huo huo tumerahisisha mahitaji mengi na utaratibu. Wakati huo huo, tumeongeza shughuli na mazoezi mengi ya kielimu na kuboresha ambayo tayari yapo ili kuhakikisha mikutano haichoshi na inabaki na uzingatiifu wa kielimu.  

Kitabu hiki kinakusanya na kupanga taarifa zote za wiki zinazohusu klabu ( wiki.agoraspeakers.org ) kwenye sehemu moja. Imebuniwa kitaalam zaidi na inaweza aidha kupakuliwa kama kitabu cha mtandaoni au kinaweza kununuliwa kupitia Amazon kwa wale ambao wanataka kitabu chenyewe. Hata hivyo, Wiki, daima itabaki kuwa chanzo chenye taarifa zote mpya za Agora, na pia chanzo cha ukweli kwenye masuala ya mtafaruku kwenye toleo lolote lililochapishwa au lililopakuliwa, kwahiyo tafadhali rejea kwenye Wiki kwa ajili ya habari mpya na mabadiliko. Toleo jipya la Mwongozo kwa lugha tofauti inaweza kupakuliwa kutoka https://wiki.agoraspeakers.org/ebooks.

Kama kawaida, tunakaribisha maoni yote, mapendekezo, ukosoaji, mawazo yote, na haswa hadithi zako - tuambie visa vya kusisimua vya klabu yako, mafanikio yako, nini umejifunza ndani ya Agora na ni jinsi gani imekusaidia. Labda kwenye mwongozo ujao, picha yako inaweza kuwepo kwenye moja ya sura zetu.

Jisikie huru kututumia ujumbe kwenda info@agoraspeakers.org au kwenye moja ya kurasa zetu za mitandao ya kijamii (angalia kipengele cha "Jinsi ya Kuwasiliana Nasi")

Agosti 21, 2021, itakuwa ni mwaka wa 5 wa kuanzishwa kwa Agora. Tumetoka mbali sana tangu ndoto ya Agora ilivyoanza mwaka 2016 na klabu moja tu mjini Madrid. Klabu hiyo moja baadae iliungwa na Gorzów Wielkopolski (Poland), alafu nyingine Visakhapatnam (India), alafu Kathmandu (Nepal)... Orodha ikaendelea kuongezeka na kuongezeka jinsi tulivyoendelea kupata rangi ramani ya dunia na rangi za Agora, kila klabu ikiongeza haiba yake yenyewe na utajiri kwenye chungu. Kwenye kitabu hiki, tumejaribu kuonesha hiko kwa kutumia picha halisi kutoka mikutano ya kiuhalisia, na ya kweli - hamna waigizaji, hamna picha zilizopangwa, hamna photoshop. Mwongozo unawakilisha jinsi haswa Agora ilivyo kwenye ukweli na utofauti wetu.

Moja kati ya vitu vikuu vinavyoendesha juhudi na mikakati ya Agora imekuwa ni kuamini kuwa kila mmoja ana mbegu za kuwa kiongozi mkubwa na nguvu ya jambo jema duniani. Mbegu hizi zinahitaji kukua tu kwenye mazingira mazuri, mafunzo sahihi, kuanzisha mahusiano mazuri na kutoa zana nzuri kwa ajili ya kushamiri. Na hapo ndipo haswa Agora inapoingia: jamii imara, yenye afya, stahimilivu, saidizi, na rafiki ambayo inawezesha uelewa wa pamoja, kujifunza kwa pamoja, na ukuaji wa kibinafsi na kitaaluma.

Kwasababu hii, mwongozo huu unaweka alama ya hatua muhimu. Itakuwa mara ya kwanza nyenzo zote za Agora kupatikana kwa lugha 30. Kutoka Kiingereza mpaka Kikorea, kutoka Kithai mpaka Kiswahili, kutoka Kijerumani mpaka Kitamil, kutoka Kihindi mpaka Kireno, ili kufikia kona zote za dunia ambapo watu wanaweza kufaidika na kile ambacho tunaweza kutoa.

Mabadiliko mengi yanakuja. Tutaendelea kupanua kile tunachokitoa kielimu na kutoa hata huduma zaidi kwa wanachama na kwa wakati huo huo kuendelea kubaki kwenye lengo letu la kufunza kiongozi aliyopo ndani ya kila mtu. Jiunge nasi kwenye safari hii ya kusisimua, na tuweke historia pamoja.

 

Alexander Hristov

Mwanzilishi, Agora Speakers International

 

Jalada

 

"Agora inakuwezesha kuwa mtu mwenye mawasiliano mazuri na kuwa kiongozi anayejiamini ambaye atajenga dunia bora."

Kwa dhamira hii yenye malengo makubwa, Shirika la Agora Speakers International liliundwa tarehe 21, Agosti, 2016. Kitu cha msingi ambacho tunakiamini ni kuwa kuna mbegu ya uongozi ya ukweli na nguvu ya jambo jema ndani ya kila mmoja, na inahitaji mazingira sahihi na zana kwa ajili ya kukua na kushamiri. Tukiongozwa na Kanuni zetu za Msingi - Kutokuwamo, Bila Ubaguzi, Sio ya Kibiashara, Ustahimilivu, na Uaminifu wa Weledi, tunawapa wanachama wetu na mafunzo muhimu kwa ajili ya kufuata ndoto zao binafsi na za kitaaluma, na kwenye mchakato huo, kufanya mabadiliko ya muda mrefu kwenye jamii zao.

Ikiendeshwa na watu wanaojitolea wenye shauku, Agora imesambaa kufikia nchi zaidi ya 70 na maelfu ya wanachama kwa muda mfupi wa miaka michache. Ikiwa ni hisani ya kweli, Agora inatoa mpango kamili wa kielimu bure kwenye ujuzi laini zote ambazo ni muhimu kwa ajili ya mafanikio, na mtandao mkubwa wa kimataifa wa klabu ambapo wanachama wetu wanaweza kukutana, kufanya mazoezi, na kujifunza kwa pamoja kwenye mazingira ya kirafiki na saidizi. Wakati wa safari yetu, wanachama wetu wameshiriki na kuongoza miradi ya dunia ya kweli ambayo ina matokeo ya muda mrefu kwa jamii zake.

Toleo hili la tatu la "Mwongozo wa Agora" lina kila kitu kuhusu Shirika la Agora Speakers International: sisi ni wakina nani, tunafanya nini, jinsi gani unaweza kushiriki kwenye klabu zetu, na hata jinsi ya kuanzisha na kuendesha klabu.

 


Contributors to this page: zahra.ak and agora .
Page last modified on Thursday August 19, 2021 17:40:06 CEST by zahra.ak.