Loading...
 

Malipo ya Uanachama

 

Muundo wa Kiuchumi wa Agora

 

Muundo wa Agora wa Kujiendeleza unahimiza kutegemea michango, ruzuku za jimbo, na mauzo ya bidhaa au huduma ya kiwango cha juu kuliko ada za uanachama. Tunapokea pia fedha kutoka asilimia ya mapato ya matukio ya kati ya klabu za Agora duniani kote.

Tunafuata mtindo sawa na Open Source: Kama unatumia mfumo wetu, nyezo, miundombinu, na huduma lakini fanya hivyo kwenye klabu za umma ili kila mmoja kwenye jamii yake anaweza akafaidai, hautolipa chohocte. Lakini, unataka kutumia vyote vilivyotajwa lakini kwa kundi la watu fulani tu, una chaguo la aidha kulipa ada ya uendeshaji ya klabu au kurudisha (kwa jamii) kwa kujiandikisha kwenye fursa zozote za kuondoa ada.

 

Ada zinazolipwa na wanachama

 

Kama mwanachama, unalipa tu ada kwa klabu ambazo umo kama wameamua kukusanya. Baadhi ya klabu ni bure; nyingine zinahitaji malipo ili kuchangia kwenye uendeshaji.

Ni maamuzi ya kila klabu kuamua kama watatoza ada au la, kiasi ambacho kitatozwa, na kwa muda gani. Ada hizi - kama zipo - zinalipwa na kusimamiwa moja kwa moja na klabu na zitatakiwa kutumiwa tu kwa ajili ya uendeshaji wa klabu kwa ujumla.

Ili kuhakikisha uangavu, uwajibikaji, na matumizi yanayofaa ya fedha, klabu ambazo zinatoza ada lazima zifuate masharti yote kwenye kipengele cha Fedha za Klabu.

Ukiachana na ada za klabu, wanachama wanaweza wakatakiwa kulipa ada ndogo kwa ajili ya kugharimia matukio ya kati ya klabu kama vile mashindano na mikutano mikubwa/makongamano. Ada hiyo inaweza ikarudishwa baadae pale tukio litakapoisha, ikitegemea matokeo ya mwisho. Tafadhali angalia kipengele cha Fedha za Klabu kwa taarifa za kina.

 

Ada zinazolipwa na klabu

Ada zinazolipwa na klabu kwenda Agora Speakers International zinategemea aina ya klabu:

Ada za klabu - 2021-2022
Aina ya Klabu Ada ya mara moja ya kuanzisha (Kuandikisha) Ada ya kila mwanachama Kiwango cha chini cha ada ya klabu kwa mwaka
Klabu ya Umma (inajumuisha klabu za vijana) 0 0 Haihusiani
Klabu za Manufaa ya Umma 0 0 Haihusiani
Klabu yenye Kizuizi 0 $42 kwa mwaka $336 (wanachama 8)
Klabu ya Shirika $100 $54 kwa mwaka $648 (wanachama 12)

 

Ada ya kiwango cha chini cha klabu inalipwa wakati wa kuandikisha klabu na ni halali mpaka mwisho wa mwaka ya kielimu (Disemba 31). Ada inatozwa kulingana na miezi iliyobaki wakati wa kujiandikisha, kwa kupata idadi kamili. Ada za wanachama ambazo ni juu ya kiwango cha chini cha klabu zitalipwa wakati wanachama wanajiandikisha kwenye klabu na ni halali mpaka Disemba 31 ya mwaka wa kujiunga. Kiwango hiki kinatozwa kwa mwezi, kwa kupata idadi kamili.

Kwa mfano:

  • Klabu ya shirika inajiandikisha tarehe 15 Julai, 2020, ikiwa na wanachama 13. Tarehe 5 Agosti, wanachama watatu (3) zaidi wanajiunga, na Oktoba 1, mwanachama mwingine anajiunga. 

Ada ya mwaka wa kwanza itahesabiwa kama ifuatavyo:

  • Ya kulipwa Julai 15, 2020:   $100 (Ada ya Kuanza) + wanachama 13  x miezi 6 (Julai-Disemba) x $4,5 = $451.   (Halali kwa kipindi cha Julai 15, 2020 - Disemba 31, 2020)
  • Ya kulipwa Agosti 5, 2020:   wanachama watatu (3) x miezi mitano (5) x $4,5 = $67,5   (Halali kwa Agosti 5 2020 mpaka Disemba 31, 2020)
  • Ya kulipwa Oktoba 1, 2020:    mwanachama mmoja (1) x miezi mitatu (3) x $4,5 = $13,5      (Halali kwa kipindi cha Oktoba 1 2020 - Disemba 31, 2020)

Kama klabu itaendelea na wanachama wake wote mpaka mwakani, ada zifuatazo zitalipwa:

  • Ya kulipwa Disemba 31, 2020:  wanachama 17 x $54 = $918.    (Halali kwa kipindi cha Januari 1,2021 - Disemba 31, 2021)

 

Mwaka 2021 na ukizingatia suala la janga linavyoendelea, ada zote za Klabu zenye Vizuizi zimeondolewa. 
Ukizingatia kuwa Shirika la Agora linatoa nyenzo zote na huduma mara moja (kwa haraka) kwa klabu zenye Vizuizi na klabu za Shirika na wanachama wake binafsi, hatuwezi kurudisha fedha kama aidha klabu ama mwanachama binafsi akiamua kuwa anataka kumaliza au kutokuwa mwanachama kabla ya muda kuisha.

 

Nyenzo za Kielimu

Kufikia matoleo ya Nyenzo za Kielimu kidijitali (mtandaoni) ni bure kwa wanachama wote wa Agor bila kujali aina ya klabu ambayo wamo na bila kujali kama klabu inatoza ada au la. Tafadhali kumbuka kuwa nyenzo hazitaki kuwekwa kwenye tovuti tofauti.

Kwa kuonegezea, Sera za Hakimiliki zinahusika hapa, wanachama wanaweza wakapakua na kutoa chapa nyenzo zozote zile kwa ajili ya kutumia ndani ya mikutano ya klabu na matukio mengine ya Agora (kama vile mashindano, mikutano mikubwa/makongamano, nk.).    

Wanachama ambao wanataka toleo la nyenzo kama kitabu ambacho kinaonekana kitaalam zaidi wanaweza wakaagiza kutoka Amazon kwa kulipia.

Tafadhali jua kuwa Nyenzo zote za Kielimu za Agora katika utofauti wake wote na lugha zote ni Hakimiliki ya Shirika la Agora Speakers International.

 

Kupunguziwa ada kwa wanachama waliomo kwenye Klabu zenye Vizuizi zaidi ya moja


Kama wewe ni mwanachama wa klabu zenye Vizuizi kabla ya moja, klabu zinahitaji kulipa ada yako kwenda Agora Speakers International mara moja tu.

Hii haitumiki kwa uanachama kwenye klabu za Shirika zaidi ya moja au uanachama wa kujumuisha kwenye klabu zenye vizuizi na za shirika kwasababu Agora inawapa klabu za Shirika seti ya gharama za huduma kwa kila mwanachama ambayo inatakiwa kulipwa kwa shirika.

 

Kuondolewa ada kwa Klabu za Shirika na Klabu zenye Vizuizi

Klabu mpya za Shirika au zanye Vizuizi wanaweza wakaondolewa ada kwa muda usiozidi miaka miwili kupitia utaratibu wa "Ulezi wa Klabu", ambapo wanaunda na kuwa walezi wa Klabu mpya ya Rejea kwenye eneo lao: 

  • Klabu hiyo mpya inatakiwa kuwa na vigezo vyote vya Klabu ya Rejea. Ada iliyosamehewa itaendelea hivyo kama vigezo vyote vimezingatiwa.
  • Klabu hiyo mpya lazima iwe bure. Gharama zozote za uendeshaji kama vile kutoa nakala, kupiga chapa fomu za uthathmini, nk, lazima zilipiwe na klabu yenye vizuizi.
  • Klabu hiyo mpya lazima iwe kwenye mji sawa na klabu ya Shirika au yenye Vizuizi.
  • Klabu hiyo mpya lazima ianzishwe japo wiki moja kabla ya klabu ya Shirika au yenye Vizuizi.
  • Wanachama wa klabu za Shirika au zenye VIzuizi lazima waingilie kusahihisha matatizo yoyote yale.
  • Wanachama wa klabu za Shirika au zenye Vizuizi lazima wahakikishe (kwa kuhudhuria wenyewe) kuwa kila kipindi cha klabu ya wazi ina japo watu 12 wanahudhuria.
Klabu inayodhaminiwa lazima iwe klabu ambayo inakutana uso kwa uso tu, bila kujali asili ya klabu inayodhamini. Ada haziwezi kuondolewa kwa ulezi wa klabu kama klabu ni ya mtandaoni au ya iliyopo nusu mtandaoni.

Contributors to this page: agora and zahra.ak .
Page last modified on Monday August 30, 2021 01:43:27 CEST by agora.